TANGAZO


Tuesday, February 11, 2014

Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif, atembelea Nungwi na Kilimani kuona uharibifu wa upepo na maji chumvi

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akitembelea sehemu inayoingia maji ya chumvi katika eneo la Kilimani mjini Zanzibar, kushoto Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Mahmoud Mohammed Mussa. 
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Zanzibar Sheha Mjaja Juma, akitoa maelezo mbele ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, kuhusiana na kuingia maji ya chumvi  katika eneo la Kilimani mjini Zanzibar.
Ofisa Tawala Mkoa wa Kaskazini Unguja Dk. Makame Ali Ussi, akitoa maelezo mbele ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, kuhusiana na kuingia maji ya chumvi katika eneo la Fungu refu, Mkokotoni. Wilaya ya Kaskazini Unguja.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akishuhudia hali ya uharibifu katika hoteli ya Zalu Nungwi, uliotokana na upepo mkali uliovuma katika Mkoa wa Kaskazini Unguja Jumapili usiku, na kusababisha majengo na maeneo kadhaa kuharibiwa vibaya.















Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akitembelea skuli ya Nungwi, kuangalia uharibifu uliotokana na upepo mkali uliovuma katika Mkoa wa Kaskazini Unguja Jumapili usiku, na kusababisha majengo na maeneo kadhaa kuharibiwa vibaya. (Picha na Salmin Said, OMKR)

No comments:

Post a Comment