Zaidi ya watu 50 wamefariki nchini Burundi baada ya kusombwa na maji pamoja na maporomoko ya udongo.
Kwa mujibu wa waziri wa usalama, mvua kubwa ilinyesha usiku kucha katika mji mkuu Bujumbura na kusababisha uharibifu mkubwa.
Waziri Gabriel Nizigama amesema kuwa tayari wamepata miili ya watu 50, waliofariki baada ya nyumba zao kuporomoka na kusombwa na maji.Majumba yamebomoka kufuatia mvua hiyo kubwa
Mitaa na vitongoji vya mji mkuu Bujumbura viliopo kaskazini vimeathirika zaidi.
Serikali ya Burundi mbali na kutangaza kwamba itagharamia mazishi na huduma kwa majeruhi, imetangaza pia siku moja ya maombolezi ya kitaifa hapo kesho.
No comments:
Post a Comment