TANGAZO


Wednesday, February 26, 2014

Kongamano la Viongozi wa Dini, Mikoa ya Lindi na Mtwara lafanyika

Mwenyekiti wa maandalizi ya Kongamano la Viongozi wa Dini mikoa ya Lindi na Mtwara MohamedSenani akiwakaribisha wajumbe katika kongamano la viongozi hao katika ukumbi wa VETA mjini Mtwara. Kongamano ambalo viongozi hao walijadiliana juu ya rasilimali za gesi asilia, mafuta na madini kwa amani na maendeleo ya Tanzania.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi akizungumza na viongozi wa dini kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara wakati wa kongamano la viongozi hao lililohusu rasilimali zetu za gesi asilia, mafuta na madinikwa amani na maendeleo ya Tanzania.
Baadhi ya wajumbe wa kongamano la viongozi wa dini wakiwasili eneo la Mnazi Bay kujionea shughuli za namna visima vya gesi vinavyofanya kazi na kuzalisha gesi ambayo ni moja ya chanzo cha nishati ya umeme kwa maendeleo endelevu ya nchi yetu.
Hiki ni moja ya kisima cha gesi kilichopo Mnazi Bay eneo la nchi kavu kinachofikisha idadi ya visima vitatu ambapo kimoja kipo eneo la bahari kuu.
Baadhi ya Viongozi wa Dini kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara wakitembelea na kujionea eneo ambapo kinajengwa kiwanda cha kuchakata gesi asili eneo la Madimba ikiwa ni moja ya ratiba yaokutembelea maeneo mbalimbali wakiwa Mtwara kwenye  kongamano lao kujadiliana na kuelimishana juu ya rasilimali za gesi asilia, mafuta na madini kwa amani na maendeleo ya Tanzania.
Sheikh Abubakar Zuberi akitoa mada ya Mtazamo wa Kiteolojia/Kidini juu ya rasilimali za gesi asilia, mafuta na madini wakati wa kongamano la viongozi hao mjini Mtwara.
Mgeni Rasmi katika kongamano la viongozi wa dini na Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikana Tanzania Dkt. Jacob Chimeledya akifungua kongamano ambapo viongozi hao walijadiliana na kuelimishana juu ya rasilimali za gesi asilia, mafuta na madini kwa amani na maendeleo ya Tanzania.
Baadhi ya viongozi wa dini wakiwa katika ukumbi wa VETA Mtwara wakisikiliza mada mblimbali zilizotolewa kataka konganmano la vingozi wa dini kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara.
Baadhi ya viongozi wa dini wakiwa katika ukumbi wa VETA Mtwara wakisikiliza mada mblimbali zilizotolewa kataka konganmano la vingozi wa dini kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara. (Picha zote na Eleuteri Mangi-  MAELEZO, Mtwara)

No comments:

Post a Comment