TANGAZO


Tuesday, February 11, 2014

Bunge Kenya kukomesha 'udanganyifu'



Wabunge wa Kenya ni miongoni mwa wanaolipwa mshahara mkubwa duniani
Bunge nchini Kenya limeidhinisha mfumo mpya wa kisasa wa kuwatambua wabunge wanaohudhuria vikao bungeni kwa kutumia alama za vidole vyao.
Spika wa bunge amekanusha madai kuwa mojawepo wa sababu ya kuwekwa mitambo hiyo ilikuwa ni kukabiliana na ulaghai miongoni mwa wabunge, '' nigependa kurekebisha dhana iliyojengwa na vyombo vya habari kwamba mitambo hii imewekwa ili kuzuia ulaghai.
Kumekuwa na tuhuma kwamba wabunge wamekuwa wakitumia afisa wa serikali kuwatilia saini kwa niaba yao ili wapate malipo ya dola 58 ya kuhudhuria vikao hivyo.Mitambo hii itasaidia katika kuokoa muda unaotumiwa na wabunge kupiga foleni ili waweze kuweka saini ya kuingia bunge kwa njia ya kawaida.''
Wabunge wa Kenya ni miongoni mwa wabunge wanaolipwa mishahara mikubwa zaidi duniani.
Mwandishi wa BBC Odeo Sirari aliyehudhuria uzinduzi huo katika majengo ya bunge Nairobi, ameona wabunge wakijisajili kwa kutumia mbinu hiyo mpya kabla ya kuanza vikao vya Jumanne ambapo wamerejea kazini tangu likizo ya Krismasi.
Wabunge hao wana hadi wiki moja kujisajili na watalazimika kutumia mashine hizo wakati wakipanga foleni kuingia bungeni.

No comments:

Post a Comment