* Yatoa msaada wa vifaa vya Hospitali, vyenye thamani ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili na Amana
Mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Meck Sadick akikata utepe kuashilia uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Mandela Road. Kwanza kushoto ni Meneja wa NMB kanda ya Dar es salaam, Bw. Salie Mlay na kwanza kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Huduma kwa wateja wakubwa NMB, Bw.Gerald Kamugisha wakishuhudia ufunguzi huu uliofanyika jana jijini Dar es salaam.
NMB yazindua tawi jipya barabara ya Mandela mkoani Dar es Salaam. Hili ni tawi la ishirini na tatu kufunguliwa katika mkoa wa Dar es Salaaam, na hii inafanya NMB kuwa benki yenye matawi mengi zaidi Tanzania, ikiwa na matawi zaidi ya 150 yaliyosambaa nchi nzima.
Meneja wa NMB kanda ya Dar es salaam, Bw. Salie Mlay akimwelezea Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (kwanza kushoto ,Bw. Meck Sadick huduma mbali mbali zitolewazo na tawi jipya la NMB mandela Road.
Tawi hili la NMB Mandela Road, linatoa huduma mbali mbali za kibenki ikiwemo akaunti za akiba, mikopo , huduma za fedha za kigeni, kukusanya mapato na kulipia kwa niaba ya serikali na taasisi mbalimbali. Tawi hili litakua wazi kila Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa kumi na nusu jioni ( 2:30 asubuhi - 10:30 jioni) na Jumamosi kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa sita na nusu mchana (8:30 asubuhi- 6:30 jioni), Jumapili na siku za sikukuu hakutakuwa na huduma ndani ya tawi hili.
Katika kusherehekea ufunguzi rasmi wa tawi hili, Benki ya NMB ilitoa msaada kwa jamii wa vifaa vya hospitali vyenye thamani ya shilingi milioni kumi ili kuunga mkono jitihada za serikali na wananchi katika kuboresha huduma katika sekta ya afya. Msaada huu unatolewa kwa hospitali ya Amana pamoja na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
No comments:
Post a Comment