Naibu Waziri wa viwanda nchini Libya ameuawa kwa kupigwa risasi
wakati alipokuwa ziarani mjini Sirte Mashariki mwa Tripoli ambako alizaliwa.
Vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa watu wasiojulikana walimfyatulia
risasi kadhaa Hassan al-Droui karibu na soko rasmi mjini humo.Libya imekuwa ikikumbwa na vurugu tangu kuondolewa mamlakani kwa hayati Muammar Gaddafi mwezi Oktoba mwaka 2011.
Sirte ilikuwa ngome ya mwisho ambako mapigano yalitokea wakati wa harakati za mapinduzi ya Muamar Gaddafi ambaye alikamatwa na kupigwa risasi akijaribu kujificha kutoka kwa waasi.
Bwana al-Droui alikuwa mwanachama wa zamani wa baraza la mpito lililosimamia kipindi cha mpito baada ya Gadaffi kuuawa.
Aliteuliwa kama naibu waziri na waziri mkuu wa kwanza wa mpito na kuendelea kushikilia wadhifa huo hata baada ya Ali Zeidan kuchukua mamlaka.
No comments:
Post a Comment