TANGAZO


Tuesday, January 7, 2014

Waziri wa Habari Dk. Fenella Mukangara azindua Baraza Jipya la Kiswahili

Wanakikundi cha fataki wakitoa Igizo kwa njia ya ushairi lililosisitiza matumizi bora ya lugha ya Kiswahili kwa maendeleo ya lugha hiyo, Afrika na duniani kwa ujumla, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Baraza jipya la Kiswahili, iliyofanyika katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa leo jjini Dar es Salaam.
Wanakikundi cha fataki wakimsalimia Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara (aliyesuka), wakati wa hafla ya uzinduzi Baraza jipya la Kiswahili leo jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara hiyo Profesa Hermas Mwansoko, kushoto kwake ni Mwenyekiti mpya wa baraza hilo, Bi. Martha Qorro na wa mwisho ni Makamu Mwenyekiti, Omar Kiputiputi.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara (kulia), akiteta jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni wa wizara hiyo, Profesa Hermas Mwansoko, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Baraza Jipya la  Kiswahili leo, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara akimpa zawadi Mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa kutumikia Baraza la Kiswahili, Suleiman Hegga wakati wa hafla ya uzinduzi wa Baraza jipya la Kiswahili leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa kulitumikia Baraza la Kiswahili, Suleiman Hegga akitoa hotuba na kuwataka wajumbe wa Baraza la Kiswahili kushikamana na kuendeleza yale waliyoanza ili kukiletea Kiswahili maendeleo Afrika na duniani kwa ujumla. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Hermas Mwansoko na kulia ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara.
Wajumbe wa Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA), wakimsikiliza Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo  Dk. Fenella Mukangara wakati wa hafla ya uzinduzi wa Baraza jipya la Kiswahili iliyofanyika katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa Leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara akitoa hotuba kwa wajumbe wa Baraza jipya la Kiswahili na kulitaka baraza hilo, kuendelea kushirikiana na vyombo vya habari katika kutoa elimu ya matumizi fasaha ya Kiswahili sanifu ili kupunguza upotoshwaji wa matumizi ya lugha ya Kiswahili. Kulia ni Mwenyekiti mpya wa Baraza la Kiswahili Martha Qorro.
Wajumbe na viongozi wapya, wakiwa kwenye picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment