Aliyekuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Ali Mwinyi (kushoto), ambaye sasa ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), akizungumza wakati wa hafla ya kumkabidhi Ofisi ya undeshaji wizara hiyo, Waziri mpya, ambaye alikuwa Naibu wake, Dk. Seif Rashid (kulia), Dar es Salaam jana. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Aliyekuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Ali Mwinyi (kushoto), ambaye sasa ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), akizungumza wakati wa hafla ya kumkabidhi Ofisi ya undeshaji wizara hiyo, Waziri mpya, ambaye alikuwa Naibu wake, Dk. Seif Rashid (katikati), Dar es Salaam jana. Kulia ni Naibu waziri, Kebwe Kebwe.
Waziri Dk. Hussein Mwinyi, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya Wakuu wa Idara na Wakurugenzi wa Wizara ya Afya wakifuatilia na kuweka kumbukumbu zao vizuri kwenye dayari zao.
Baadhi ya Wakuu wa Idara na Wakurugenzi wa Wizara ya Afya wakifuatilia na kuweka kumbukumbu zao vizuri kwenye dayari zao. Wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Charles Pallangyo na wa pili ni Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Donald Mmbando.
Waziri Dk. Hussein Mwinyi (kulia), ambaye sasa ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), akizungumza katika hafla hiyo. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Charles Pallangyo na kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Donald Mmbando.
Waziri Dk. Hussein Mwinyi na Waziri Dk. Seif Rashid (wote katikati), wakizungumza katika hafla hiyo.
Waziri mpya wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid (kulia), akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano ya Ofisi (Wizara), Dar es Salaam jana.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Kebwe S. Kebwe akizungumza katika hafla hiyo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Kebwe S. Kebwe akizungumza katika hafla hiyo. Kushoto ni Kiongozi wake, Waziri Dk. Seif Rashid.
Waziri Dk. Hussein Mwinyi (kushoto) na Waziri Dk. Seif Rashid, wakisaini makabidhiano hayo, wizarani hapo jana
Waziri Dk. Hussein Mwinyi (kushoto) na Waziri Dk. Seif Rashid wakisaini makabidhiano hayo, Dar es Salaam jana. Kulia ni Naibu Waziri, Kebwe Kebwe.
Aliyekuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi (kushoto), ambaye sasa ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, akimkabidhi makabrasha ya undeshaji Ofisi Waziri mpya wa wizara hiyo, ambaye alikuwa Naibu wake, Dk. Seif Rashid wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi wizarani hapo, Dar es Salaam jana.
Aliyekuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi (kushoto), ambaye sasa ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, akimkabidhi makabrasha ya undeshaji Ofisi Waziri mpya wa wizara hiyo, ambaye alikuwa Naibu wake, Dk. Seif Rashid wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi wizarani hapo, Dar es Salaam jana. Kulia ni Naibu waziri, Kebwe Kebwe.
Aliyekuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Ali Mwinyi (wa pili kushoto waliokaa), ambaye sasa ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), akiwa na aliyekuwa Naibu wake, ambaye sasa ni Waziri wa wizara hiyo, Dk. Seif Rashid (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na viongozi na wakurugenzi wa vitengo mbalimbali wa wizara, mara baada ya makabidhiano hayo jana.
Waziri Mwinyi akiagana na Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kebwe S. Kebwe.
Na Catherine Sungura-MOHSW
Aliyekuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi kwasasa ni Waziri wa Ulinzi na JKT amewataka mawaziri wapya wa wizara hiyo kupitia muundo wa wizara na utekelezaji wake ili kuweza kukabiliana na changamoto zilizopo katika sekta hiyo.
Hayo alisema jana wakati wa kukabidhi ofisi kwa waziri mpya wa afya na ustawi wa jamii Dkt, Seif Rashid ambaye anachukua nafasi hiyo baada ya Rais JAKAYA KIKWETE kufanya Mabadiliko ya Baraza la Mawaziri na Naibu wake Dk. Kebwe Kebwe.
Dk. Mwinyi alisema wakati anaingia wizara hiyo kulikuwa na changamoto nyingi hivyo ili kuweza kufanikisha ni pamoja na kutembelea miradi yote iliyopo chini ya wizara hiyo ili kuweza kutimiza malengo ya utekelezaji wa serikali iliyopo madarakani.
“Nilivyofika wizarani hapa niliulizwa nini changamoto ya sekta hii, hivyo ni wakati wenu sasa mpate fursa ya kupitia na kutembelea miradi hiyo na kuisaidia sekta hii kupiga hatua kwa kasi", alisema.
Alizitaja changamoto kuu nne zinazoikabili sekta ya afya nchini ni pamoja na uhaba wa watumishi wa afya ambapo wakati wa kipindi chake waliweza kuajiri watumishi 7,000 hivyo amewataka kutimiza malengo ya kuajiri watumishi wapatao 10,000 kwa mwaka kufikia mwaka 2015.
Changamoto nyingine ni ile ya uhaba wa dawa na vitendea kazi, Dk. Mwinyi aliwataka watafute mkakati wa kutatua upotevu wa dawa kwa kuisimamia Bohari ya dawa (MSD) ili dawa ziweze kufika kwenye vituo vya kutolea huduma bila kupotea na kwa wakati.
Aidha, aliainisha changamoto nyingine ni uhaba wa bajeti na ule wa mfumo wa kieletroniki(health information System) ambazo zikifanikiwa zitasaidia kupunguza ama kuondoa kabisa tatizo la watanzania kupata huduma za afya nchini kwa kutumia bima ya afya na wafanyakazi wa kada za afya.
Kwa upande wake Waziri Mpya Dk. Seif Rashid ambaye awali alikuwa na Naibu waziri wa wizara hiyo amesema wataendelezeza mipango yote iliyoachwa na Waziri Mwinyi lengo ni kuhakikisha kero zote zilizopo katika sekta hiyo zinatatuliwa na kuahidi kuzifanyia kazi maeneo yote manne kwa kushirikiana na watumishi wa sekta hiyo.
No comments:
Post a Comment