TANGAZO


Wednesday, January 8, 2014

Waumini wauawa msikitini Nigeria

 


Watu waliojihami wameshambulia msikiti katika jimbo la Kano Kaskazini mwa Nigeria na kuwaua waumini watatu huku wakiwajeruhi wengine 12.
Polisi wanasema kuwa watu hao waliwafyatulia risasi waumini waliokuwa msikitini katika kijiji anakoishi gavana wa jimbo hilo, Rabiu Musa Kwankwaso.
 
Babake gavana huyo alikuwa msikitini ingawa alinusurika kifo.
Hakuna mtu aliyewajibikia mashambulizi hayo lakini mmoja wa wasaidizi wa bwana Kwankwaso alisema kuwa shambulizi hilo lilikuwa la kulipiza kisasi hatua ya gavana huyo kuhama chama tawala.
Kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Boko Haram, pia lilifanya mashambulizi kadhaa kama hayao mjini Kano, na katika maeneo mengine mbali mbali Kaskazini mwa Nigeria.
Haijulikani ikiwa Rais Goodluck Jonathan wa chama cha PDP atawania tena urais mwaka ujao.
Kipindi hiki ambapo watu wana hamasa z akisiasa hukumbwa na visa kama hivi vinavyotokana baina ya makundi hasimu ya kisiasa.
Bwana Kwankwaso alikuwa miongoni mwa watu watano mashuhuri waliokihama chama cha PDP na kujiunga na chama cha upinzani cha All Progressives Congress mnamo mwezi Novemba.
Heshimu Suleiman, msaidizi maalum wa gavana huyo alisema kuwa, shambulizi hilo lilinuiwa kumuadhibu bwana Kwankwaso kwa kukihama chama tawala.
Hata hivyo chama cha PDP bado hakijatoa tamko lolote kuhusiana na madai hayo.
Mnamo mwezi Disemba, rais wa zamani wa Nigeria,Olusegun Obasanjo alisema itakuwa kwenda kinyume na maadili kwa Rais Jonathan kuwania tena urais mwaka ujao.
Alisema Rais Jonathan ameshindwa kushughulikia matatizo yanayokumba Nigeria ikiwemo Ufisadi na hata kushindwa kukabiliana na kundi la wapiganaji la Boko Haram ambalo limekuwa likifanya mashambulizi ya mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment