Wajumbe wa pande mbili zinazopigana vita nchini Syria
wanaohudhuria mkutano wa amani mjini Geneva walikutana kwa muda mfupi.
Walikaa chumba kimoja huku wamekabiliana, lakini hawakuzungumza moja-kwa-moja
isipokuwa kwa kuptia mpatanishi wa Umoja Mataifa, Lakhdar Brahimi.Kikao hicho cha kwanza kilidumu nusu saa tu, na mpatanishi pekee ndiye aliyezungumza.
Mwandishi wa BBC mjini Geneva anasema utaratibu huo umewekwa ili kuepusha ugomvi kati ya wajumbe; na itifaki hiyo itafuatwa katika vikao vijavyo.
Wajumbe wakitarajiwa kukutana tena Jumamosi, na watalenga namna ya kufikisha misaada kwa wanyonge na kuwaachilia huru wafungwa wa kisiasa.
Upinzani unasema utaomba kuwa mapigano yasitishwe katika mji wa Homs.
No comments:
Post a Comment