Watu waliojihami katika mji wa Karachi nchini Pakistan,
wamewaua kwa kuwapiga risasi wahudumu watatu wa afya wakiwemo wanawake wawili
waliokuwa wanatoa chanjo ya Polio.
Hili ni shambulizi la hivi karibuni likiwalenga wahudumu wa afya wanaotoa
chanjo ya Polio au ugonjwa wa kupooza.Mwanamke mmoja alifariki papo hapo wakati mwingine alifariki akipelekwa hospitalini.
Shambulizi hilo ni pigo kubwa kwa juhudi za Pakistan kupambana na ugonjwa huo unaolemaza.
Kando na Afghanistan na Nigeria, Pakistan ni moja ya nchi ambako ugonjwa wa Polio ni janga kubwa.
Wapiganaji wa Taliban wanapinga chanjo ya ugonjwa wa kupooza na wamekiri kuwaua wafanyakazi wa afya wanaotoa chanjo hiyo nchini Pakistan.
No comments:
Post a Comment