Baada ya mjadala mkali, kundi la upinzani nchini Syria
limekubali kuhudhuria mazungumzo ya amani mjini Geneva wiki ijayo.
Uamuzi huo ulipokelewa vyema na wafadhili wake wa Magharibi waliosema ni
hatua muhimu huku wakionyesha matumaini katika mazungumzo hayo.Swala la iwapo kuna umuhimu wa kuhudhuria mazungumzo hayo yaliugawanya upinzani huo huku wengi wa wanachama wa kundi hilo wakiamua kujiondoa.
Mwandishi wa BBC amesema kuwa kutakuwa na maswala mengi kuhusu vile wawakilishi wa upinzani huo walivyojitayarisha.
Wakati huohuo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry amepongeza uamuzi wa upinzani wa Syria kwenda kwa mazungumzo nchini Switzerland.
Lengo la mkutano ni kuona ikiwa inawezekana kuunda serikali ya mpito, ili kumaliza mzozo wa Syria.
Mgogoro huo wa miaka mitatu, umesababisha vifo vya zaidi ya watu 100,000
No comments:
Post a Comment