TANGAZO


Wednesday, January 22, 2014

Ugonjwa wa Surua tishio Guinea

 


Ugonjwa wa surua unaelezwa kuwa hatari kwa Watoto
Shirika la kimataifa linaloshughulikia maswala ya Watoto UNICEF, limeanza kuandaa kampeni ya chanjo kwa Watoto zaidi ya milioni 1.6 kupambana na ugonjwa wa Surua uliojitokeza nchini Guinea, Ripoti zikieleza watoto wengi wameugua ugonjwa huo hasa mjini Conakry.
Tangu Mwezi Novemba mwaka jana, Watoto 37 mjini Conakry, wote wakiwa nchini ya umri wa miaka 10 wamethibitishwa kuwa na ugonjwa huo.
Hali hii imeisukuma Wizara ya Afya nchini Guinea kutangaza kutokomezwa kwa mlipuko wa maradhi hayo katika maeneo mbalimbali ya mji wa Conakry, Matam, Matoto na Ratoma.Katika kipindi cha majuma kadhaa yaliyopita, ripoti zimesema kuwa ugonjwa huo umeongezeka kwa kasi na kusababisha kifo cha mtoto mmoja.
Ugonjwa huu pia umeripotiwa katika maeneo mengine ya nchi hiyo, Boke,Coyah ,dubreka, Kissidougou na Mandiana.
Mwakilishi wa UNICEF nchini Guinea, Dr.Mohamed Ayoya ametoa tahadhari kuwa ugonjwa huu ni hatari katika mji wenye Watu wengi kama Conakry kwani ugonjwa wa Surua husambaa kwa kasi.
Serikali ya Guinea,UNICEF, Shirika la afya duniani (WHO) na shirika la madaktari wasio na mipaka, (MSF) wanaunganisha nguvu kutafuta namna ya kupambana na mlipuko huo.
UNICEF itatoa dawa za chanjo, majokofu, sindano , vifaa vingine vya kitabibu kwa Serikali kwa ajili ya chanjo ya Watoto katika maeneo ya Kaloum na Dixinn ya mjini Conakry na maeneo mengine ya nje ya mji huo yaliyoathiriwa na ugonjwa wa Surua.
Kampeni ya kitaifa ya chanjo dhidi ya Surua itaanza majuma kadhaa yajayo baada ya kupatikana kwa vifaa na fedha.
Halikadhalika UNICEF na Washirika wake watatoa dawa kwa Serikali kuwatibu Watoto walioathirika na ugonjwa huo.

No comments:

Post a Comment