Wapatanishi katika mgogoro wa Sudan Kusini wanasema kuwa waasi
nchini Sudan Kusini wanatarajiwa kutia saini mkataba wa kusitisha vita na
serikali ya Rais Salva Kiir baadaye leo mjini Addis Ababa Ethiopia.
Wapatanishi kutoka shirika la IGAD, wamedokeza kuwa mkataba huo utatiwa saini
katika hafla maalum mjini Addis Ababa.Aidha mkataba huo utasitisha vita vya mwezi mmoja vilivyoanza tarehe 15 Disemba mwaka jana kati ya waasi na serikali.
Mazungumzo ya amani yamekumbwa na matatizo kuhusu swala la wafungwa 11 wa kisiasa ambao bwana Riek Machar anayeongoza waasi alitaka waachiliwe kama sharti la kutia saini mkataba wa amani.
Wiki jana wanajeshi wa serikali walifanikiwa kukomboa miji kadhaa iliyokuwa imetekwa na waasi.
Zaidi ya watu 500,000 wamelazimika kutoroka makwao kutokana na vurugu hizo za mwezi mmoja.
No comments:
Post a Comment