*Awataka wafanyabiashara kuwafikiria wananchi
Baadhi ya Viongozi na wananchi waliohudhuria katika ufunguzi wa Tamasha la Biashara (Shopping Festival) katika Viwanja vya Maisara Suleiman, Mkoa wa Mjini Magharibi jana, lililofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein.
Wafanyakazi mbalimbali wa maidara na Tasisi binafsi wakiwa katika Tamasha la Biashara (Shopping Festival), lililoanza jana na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, katika Viwanja vya Maisara Suleiman, Mkoa wa Mjini Magharibi jana.
Wananchi wakiangalia bidhaa katika banda la Shirika la ZSTC wakati wa Tamasha la Biashara (Shopping Festival), lililoanza jana na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya Maisara Suleiman, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Wananchi wakipata maelezo katika banda la Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC, wakati wa Tamasha la Biashara (Shopping Festival), lililoanza jana na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya Maisara Suleiman, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akibonyeza kitufe cha king'ora wakati alipolizindua Tamasha la Biashara (Shopping Festival), lililoanza jana katika viwanja vya Maisara Suleiman, Mkoa wa Mjini Magharibi. Kushoto ni Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi na kulia ni Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko, Nassor Ahmed Mazrui.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akiapata maelezo alipotembelea banda la Benki ya Posta Tanzania (Western Union), wakati wa Tamasha la Biashara (Shopping Festival), lililoanza jana katika viwanja vya Maisara Suleiman, Mkoa wa Mjini Magharibi, mara baada ya kulifungua.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mwendeshaji, Mwanahija Almasi Ali, alipotembelea banda la Shirika la ZSTC, wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Biashara (Shopping Festival), lililoanza jana katika viwanja vya Maisara Suleiman, Mkoa wa Mjini Magharibi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ametahadharisha juu ya tabia ya baadhi ya wafanyabiashara nchini kutumia fursa zitolewazo na Serikali kuwapunguza wananchi makali ya maisha kujinufaisha wao binafsi.
Ametaja hatua kama za kupunguza, baadhi ya wakati, ushuru wa bidhaa kwa lengo la kukabiliana na mfumuko wa bei hutumiwa vibaya na wafanya biashara kwa kuweka bei zisizolingana na unafuu huo hivyo kunufaika wao na kuwaacha wananchi wakihangaika na ugumu wa maisha kutokana na bei kubwa za bidhaa.
Dk. Shein ametoa tahadhari hiyo jana wakati akifungua Tamasha la Biashara la Mwaka 2014 lililoandaliwa kwa pamoja kati ya Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania-TANTRADE kwenye viwanja vya Maisara mjini Unguja.
Amebainisha kuwa vitendo vya wafanyabiashara hao sio tu vinaathiri mwenendo mzima wa uchumi wa nchi ikiwemo ulipaji wa mishahara lakini pia vinaharibu uhusiano mzuri kati ya wananchi na Serikali yao.
Kwa hiyo aliwataka wafanyabiashara kuunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali katika kuendesha biashara na uchumi na kurejea wito wake wa kuwataka wafanyabiashara hao kulipa kodi kama inavyotakiwa kisheria kulingana na leseni na biashara wanazifanya.
Hata hivyo katika hotuba yake hiyo Dk. Shein alieleza kutiwa moyo na mwamko mpya miongoni mwa wafanyabiashara wa kulipa kodi kwa hiari na kwa uadilifu hali ambayo alisema imechangia kunyanyua kiwango cha makusanyo ya Serikali kwa mwezi hivyo kuiwezesha kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Halikadhalika amesifu hatua ya baadhi ya wafanyabiashara wakubwa nchini kujenga utamaduni mpya wa kutumia sehemu na mapato yao kuchangia utekelezaji wa shughuli za maendeleo.
Katika hotuba yake hiyo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ameeleza kufadhaishwa kwake na kuongezeka kwa matukio ya kukamatwa wafanyabiashara ndani na nje ya nchi kwa kujishughulisha na biashara zisizoruhusiwa kisheria.
Amefafanua kuwa vitendo hivyo vinaathiri na kuharibu kwa kiasi kikubwa maendeleo ya biashara nchini kwa kuwa vinajenga mazingira magumu kwa wafanyabiashara nchini hasa wanapotaka kusafiri nje ya nchi.
Kwa hivyo ametoa wito kwa wafanyabiashara nchini kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kuwafichua wafanyabiashara hao wachache ili kulinda heshma ya nchi na kunusuru maendeleo ya biashara nchini.
Wakati huo huo Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazrui amesema madhumuni ya kuandaa tamasha hilo ni kuitangaza Zanzibar kama kituo cha biashara, kuweza kuchangamsha na kuhamasisha biashara na kuongeza wigo au hisa katika soko.
Akizungumza kumkaribisha mgeni rasmi Waziri Mazrui aliyataja madhumini mengine kuwa ni pamoja na kuitangaza Zanzibar kiutalii, kupatikana bidhaa kwa bei nafuu, kuwawezeha wafanyabiashara na wazalishaji kukutana na wateja moja kwa moja na kutoa fursa kwa wazalishaji na wafanyabishara kujitangaza kibiashara.
Alisema tamasha hilo la siku saba limekusanya washiriki wapatao 160 wakiwa ni kutoka Zanzibar, Tanzania Bara, Syria, Indonesia, Misri, Malaysia, India, Pakistan, Kenya, Uganda, Burundi, Uturuki na Kituo cha Biashara cha Dubai.
Katika maelezo yake Waziri huyo alipendekeza kwa mgeni rasmi kufanyika kwa tamasha hilo kila mwaka pendekezo ambalo mgeni rasmi aliliafiki. Halfa hiyo ilihudhuriwa pia na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi.
No comments:
Post a Comment