TANGAZO


Monday, January 6, 2014

Rais Kikwete aongoza mamia ya waombolezaji kumzika Dk. William Mgimwa kijijini kwao leo

mg1Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga marehemu William Mgimwa kijijini kwake Magunga jimbo la Kalenga, Iringa, leo Januari 6, 2014.

mg2 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka shada la maua  wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga marehemu William Mgimwa kijijini kwake Magunga Jimbo la Kalenga, Iringa, leo Januari 6, 2014.
 
mg3

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete  na mkewe, Mama Salma Kikwete wakitoa heshima baada ya kuweka shada la maua wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga marehemu William Mgimwa kijijini kwake Magunga jimbo la Kalenga, Iringa, leo Januari 6, 2014.
mg4 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Godfrey Mgimwa, mmoja wa watoto wa marehemu wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga William Mgimwa kijijini kwake Magunga jimbo la Kalenga, Iringa, leo Januari 6, 2014.
mg5
Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akimfariji  Mama mzazi wa marehemu wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga William Mgimwa kijijini kwake Magunga jimbo la Kalenga, Iringa, leo Januari 6, 2014.
 
mg6
Mama Salma Kikwete   akimfariji Godfrey Mgimwa, mmoja wa watoto wa marehemu wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga William Mgimwa kijijini kwake Magunga jimbo la Kalenga, Iringa.
 
mg7
Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akimfariji  Mjane wa marehemu wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga William Mgimwa kijijini kwake Magunga jimbo la Kalenga, Iringa, leo januari 6,
mg8
Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiwapa mkono wa pole wananchi wa Kalenga  wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga William Mgimwa kijijini kwake Magunga jimbo la Kalenga, Iringa, leo Januari 6, 2014.
mg10
Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiwapa mkono wa pole machifu    wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kalenga William Mgimwa kijijini kwake Magunga jimbo la Kalenga, Iringa, leo Januari 6, 2014. (Picha zote na IKULU)


Na  Francis Godwin, Iringa
MAELFU   ya  wakazi  wa Mkoa  wa Iringa na  baadhi  ya  viongozi  wa Vyama  vya  siasa na Serikali wakiongozwa na  Rais Dk. Jakaya Kikwete, wameshiriki katika mazishi ya aliyekuwa  Mbunge wa Jimbo la Kalenga na Waziri wa Fedha Dk. Wiliam Mgimwa.
 
Huku Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika  salam zake za Serikali akielezea  jinsi ambavyo Taifa lilivyopata pigo kubwa kufuatia kifo cha Dk. Mgimwa kutokana na mchango wake  katika Baraza la Mawaziri.
 
Katika  mazishi  hayo, yaliyofanyika leo kijiji kwake Magunga  Jimbo la Kalenga   wananchi  mbalimbali   walionyesha  kujipanga  barabarani  kutoka Manispaa ya  Iringa  hadi  kijijini kwake  huku  wakiupungia mkono msafara  wa    rais Kikwete na baadhi yao  wakilazimika  kutumia  usafiri wa baiskeli na pikipiki  kwenda katika mazishi  hayo.
 
Akitoa shukrani za  familia kwa niaba ya  familia  mtoto wa marehemu Dk. Mgimwa Godfrey  Mgimwa  aliishukuru   serikali kwa  jinsi ambavyo ilivyohangaika  kumuuguza baba  yake  na  kutoa wosia  mzito wa marehemu  Dr Mgimwa ambao  alimtaka kuufikisha kwa Rais  Kikwete.
 
Alisema  katika  uhai  wake kabla  ya kifo  chake  ikiwa ni siku tano kabla  Dr  Mgimwa alimwita na  kumtaka  kufikisha shukrani zake kwa Rais  Kikwete kwa  kumtembelea mara mbili Hospital  alipokuwa amelazwa  pamoja na  spika wa bunge Anne makinda.
 
Pia  alisema  kuwa alieleza dhamira  yake ya  kuwatumikia wana Kalenga na  kusema  zawadi kubwa ni msaada wa bati  zaidi ya  2000 kwa wananchi hao  ili kuendeleza ujenzi wa shule na  vituo  vya afya  jimboni.
 
"Baba  kabla ya  kufa  aliniachia  wosia  huo juu ya wana Kalenga kwa kuwashukuru kwa ushirikiano  wao na  kutoa bati ila alipenda  kuona Kalenga  inakuwa na maendeleo zaidi"
 
Kwa  upande  wake  waziri Mkuu Pinda  alisema  kuwa  serikali imepata pigo kubwa  juu ya kifo hicho na kuwa  bado serikali  itaendelea  kuwa karibu na familia ya Dk. Mgimwa  na pale  penye tatizo  isisite  kuwasiliana .
 
Hata  hivyo  Rais  Kikwete  hakupata  kuzungumza  chochote  katika msiba  huo  zaidi ya  kuweka mchanga na shada la maua pamoja na kuwapa mkono  ndugu wa Dk. Mgimwa .
 
Spika  wa Bunge Anne Makinda  alisema kuwa  bunge  limempoteza kiongozi na mbunge aliyependa kutumia  nafasi yake kwa ajili ya Taifa  na kuwa kamwe mchango  wake  hawataacha kuukumbuka.

No comments:

Post a Comment