Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze, mkoani Pwani, Said Bwanamdogo aliyefariki juzi na kuzikwa leo, kijijini kwao Miono Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Waombolezaji wakiuteremsha ndani ya kaburi mwili wa marehemu Said Bwanamdogo, wakati wa mazishi yaliyofanyika katika kijiji cha Miono, Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani. Mazishi hayo yamehudhuriwa na viongozi mbaliombali wa Chama na Serikali.
Waombolezaji wakiuzika mwili wa marehemu Said Bwanamdogo wakati wa mazishi yaliyofanyika kijiji kwao, Miono Wilaya ya Bagamoyo,Mkoa wa Pwani leo. Mazishi hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali.
Rais Jakaya Kikwete akishika sepetu, akiweka mchanga kwenye kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Saidi Bwanamdogo, wakati wa mazishi yake katika kijiji cha Miono, wilayani Bwagamoyo, Mkoa wa Pwani leo. (Picha zote na Omary Said)
No comments:
Post a Comment