TANGAZO


Tuesday, January 7, 2014

Mwanawe mfalme mahakamani Uhispania



Mumewe mwanamfalme wa Uhispania Princes Cristina pia anachunguzwa kwa kosa la rushwa

Mwanawe wa mwisho mfalme Juan Carlos wa Uhispania amefikishwa mahakamani kwa madai ya kukwepa kulipa ushuru na ulaji rushwa.
Princess Cristina anatazamiwa kufika katika mahakama ya Majorca mwezi Machi baada ya kushukiwa kutenda kosa hilo.
Mumewe Inaki Urdangarin, amekuwa akichunguzwa kwa mwaka mzima sasa kwa kushukiwa kwa kosa la ubathirifu wa mamilioni ya Dola za umma zilizotolewa kushughulikia mradi wa kushughulikia jamii.
Amekanusha madai hayo.
Mwanahabri wa BBC anasema kesi hiyo imedhalalisha jamii ya kifalme huko Uhispania na kuibua ukosoaji chungu nzima kutoka kwa raia wa taifa hilo.

No comments:

Post a Comment