Watu wawili wameripotiwa kuuawa na wengine 20 kujeruhiwa
kufuatia mlipuko uliotokea katika ngome kuu ya kikundi cha Hezbollah katika
maeneo yanayokaliwa na waumini wa Kiislam wa madhehebu ya Shia kusini mwa Beirut
nchini Lebanon.
Televisheni ya Hezbollah ya al-Manar imeonyesha miali ikitokea katika jengo
moja la ghorofa, huku moshi mnene ukitanda angani.Televisheni ya Al-Manar imesema mlipuko huo umetokea katika mtaa wa Arid katika wilaya ya Harat Hreik.
Umati mkubwa umeonekana ukikusanyika katika eneo la tukio.
Hili ni tukio la hivi karibuni nchini Lebanon. Watu watano waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika bomu lililotokea Januari Pili katika eneo hilo la Beirut.
Waziri wa zamani Mohamad Chatah, ambaye ni wa madhehebu ya Sunni na mkosoaji wa kundi la Hezbollah, aliuawa na wengine watano kutokana na mlipuko wa bomu lililotegwa katika gari, mwezi Desemba mwaka jana.
No comments:
Post a Comment