TANGAZO

Monday, January 20, 2014

Matukio mbalimbali katika picha ya utoaji zawadi kwa washindi na ufungwaji wa michuano ya Tennis kwa Vijana wa Afrika Mashariki chini ya umri wa miaka 16 jijini Dar

Uongozi wa juu wa Chama cha Tennis Tanzania (TTA), ukiwa katika hafla ya utoaji zawadi kwa washindi mbalimbali na ufungaji wa mashindano ya mchezo huo, Afrika Mashariki kwa vijana wa umri chini ya miaka 16, katika Viwanja vya Gymkhana, jijini Dar es Salaam juzi. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Baadhi ya wachezaji wa timu mbalimbali za Afrika Mashariki walioshiriki katika mashindao hayo wakiwa katika hafla hiyo, viwanjani hapo.
Baadhi ya watendaji wa Chama cha Tennis wakiwa katika hafla hiyo.
Baadhi ya wachezaji wa timu mbalimbali wakivalishwa medali zao walizojishindia katika michuano hiyo.

Mshindi wa vijana wa chini ya umri wa miaka 14, kijana kutoka Kenya, akivalishwa medali yake ya dhahabu.
Vijana wa Tanzania wakivalishwa medali zao walizojishindia katika mivhuano hiyo.
Kijana wa Tanzania akivalishwa medali yake ya dhahabu aliyoshinda katika michuano hiyo.
Mwandishi Robert Oknda, akimvalisha medali mmoja wa wachezaji wa timu ya Kenya.

Katibu Mkuu wa TTA, William Kallaghe, amvalisha medali mmoja wa washindi wa mashindano hayo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Tennis Tanzania (TTA), William Kalaghe, akimvisha medali ya dhabu mshindi wa kwanza chini ya umri wa miaka 12 wa mchezo huo, Sarah Kassim wa Ethiopia baada ya kushinda katika mashindano ya Vijana wa Afrika Mashariki, chini ya umri wa miaka 16, wakati wa ufungaji wa mashindano hayo, Viwanja vya Gymkhana jijini juzi.
Katibu Mkuu wa TTA, William Kallaghe, akipiga picha na wachezaji baada ya kuwavalisha medali zao walizojishindia katika mashindano hayo.

Rais wa TTA, Methusela Mbajo akimvalisha medali mmoja wa washindi wa timu ya Tanzania.
Mbajo akimpongeza kijana huyo.
Uongozi wa TTA, ulioandaa mashindano hayo, Rais Methusela Mbajo (kulia), Makamu wa Rais, Fina Mango (katikati) na Katibu Mkuu, William Kallaghe wakipiga picha ya pamoja kwa ajili ya kuweka kumbukumbu yao.
Mbajo akiwakabidhi washindi wa tatu, Kenya kikombe chao cha ushindi wa tatu kaika mashindano hayo.
Ofisa Ukuzaji wa Shirikisho la Kimataifa la mchezo wa Tennis (ITF), Afrika Mashariki, Therry Ntwali (kushoto), akimkabidhi kikombe cha ushindi wa pili nahodha wa timu ya Vijana ya Tanzania, chini ya umri wa miaka 16 ya mchezo huo, Tumaini Meshuko, wakati wa ufungaji wa mashindano ya Vijana kwa nchi za Afrika ya Mashariki, Viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam juzi. Ushindi wa kwanza ulinyakuliwa na Burundi na Kenya kushika nafasi ya tatu.
Washindi wa kwanza wa michuano hiyo, Burundi wakishangilia kombe lao.
Washindi wa kwanza wa mashindano ya Tennis kwa Vijana wa chini ya umri wa miaka 16 kwa nchi za Afrika Mashariki, Burundi (katikati), wa pili Tanzania (kushoto) na wa tatu Kenya (kulia), wakiwa wamenyanyua vikombe vyao, wakishangilia baada ya kukabidhiwa wakati wa ufungaji wa  mashindano, Viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam juzi.

Makamu wa Rais wa TTA, Fina Mango, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla hiyo. Kushoto ni Rais wa TTA, Methusela Mbajo.
Timu ya Kenya wakipiga picha huku wakiwa wameshikilia kombe lao la ushindi wa tatu.
Washindi wa kwanza, Burundi wakipiga picha huku wakiwa wameshikilia kombe na medali zao.
Washindi wa Pili, Tanzania wakiwa wameshikilia medali na kombe lao la ushindi wa pili katika michuano hiyo.
Washindi wa Pili, Tanzania wakiwa wameshikilia medali na kombe lao la ushindi wa pili katika michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment