Waandamanaji kadha wameuwawa katika mapambano yaliyotokea mjini
Cairo na miji mengine ya Misri, wakati maandamano ya pande zinazopingana
yamefanywa kuadhimisha mwaka wa tatu wa maandamano yaliyompindua Hosni
Mubarak.
Inaarifiwa kuwa bomu lilotegwa kwenye gari liliripuka karibu na kambi ya polisi katika mji wa Suez.
Wafuasi wa serikali piya walikusanyika katika medani ya Tahrir kuadhimisha siku hiyo, wakipiga kelele huku wamebeba picha za mkuu wa jeshi, Jenerali Abdul Fattah al-Sisi.
No comments:
Post a Comment