TANGAZO


Thursday, January 16, 2014

Liyumba ashinda kesi ya kukutwa na simu gerezani


Mkurugenzi wa zamani wa Utawala na Utumishi (DPA) wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba ameshinda kesi ya kukutwa na simu gerezani iliyokuwa inamkabili hivi punde katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam. Liyumba ameshinda kesi hiyo baada ya upande wa Jamhuri na mchunguzi wa kesi hiyo kushindwa kuithibitishia mahakama kuhusu tuhuma hiyo. Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi, Augustina Mmbando kuanzia saa 3:30 mpaka 4:20 asubuhi.

Aliyekuwa mshistakiwa wa kukutwa na simu aina ya Nokia gereza Ukonga, Amatus Liyumba (mbele kushoto), akiondoka na ndugu zake, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, baada ya kushinda kesi hiyo katika hukumu iliyosomwa na Hakimu mkazi Agustina Mmbando mahahakamani hapo leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Amatus Liyumba (katikati mbele), akiondoka na ndugu zake, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam leo, baada ya kushinda kesi iliyokuwa ikimkabili, ya kukutwa na simu aina ya Nokia akiwa gerezani Ukonga, alikokuwa akitumikia kifungo chake.

No comments:

Post a Comment