Jeshi la Sudan Kusini linasema kuwa limeukomboa mji muhimu wa
Malakal kutoka kwa waasi.
Msemaji wa jeshi Phillip Aguer amesema kuwa vikosi vya serikali vimewatimua
waasi kutoka mji huo ambao ndio mji mkuu wa jimbo la Unity lenye utajiri mkubwa
wa mafuta.Lakini msemaji wa waasi, Brigedia-Generali Lul Ruai, amekanusha ripoti hizo ikisema kuwa waasi wangali wamuteka mji huo.
Ukombozi huu unakuja siku mbili baada ya wanajeshi kukomboa mji wa Bor.
Waandishi wa habari wanasema kwamba ikiwa ni kweli serikali imekomboa Malakal, mji wa mwisho mkubwa uliokuwa umesalia chini ya waasi, huenda hatua hiyo ikakwamua mazungumzo ya amani ya pande zote mjini Addisa Ababa, Ethiopia.
Waasi hata hivyo wangali wanadhibiti baadhi ya sehemu za nchi hiyo hasa maeneo ya vijijini.
No comments:
Post a Comment