Jengo la Kampuni ya Kusambaza Dawa ya Phillips, iliyopo Kiwalani, Dar es Salaam, likiteketea kwa moto leo. Sababu zilizopelekea kuungua jingo hilo, hazikuweza kufahamika mara moja.
Wananchi wakiushangaa moto huo, uliokuwa ukiliunguza jingo hilo.
Moto ukiendelea kuwaka huku gari la zimamoto la Uwanja wa Ndege likiendelea kuuzima
Wafanyakazi wa gari la kuzimia moto, wakiweka mpira yao ya kurushia maji vizuri kwa ajili ya kuanza kuuzima moto huo.
Moto ukiwaka kwa nguvu kubwa na hivyo kuendelea kuliteketeza jingo hilo.
Wafanyakazi wa gari la zimamoto wakiwa kazini kuuzima moto huo.
Wananchi wakishangaa huku kazi ya kuuzima moto huo, ikiendelea.
No comments:
Post a Comment