Serikali ya Sudan Kusini na wapiganaji wanaendelea kulaumiana
kwa kuvunja makubaliano ya kusitisha mapigano ambayo yalianza kutekelezwa
Ijumaa.
Msemaji wa waasi, Brigedia Jenerali Lul Ruai, alieleza kuwa wanajeshi wa
serikali wameshambulia maeneo yao katika sehemu kadha.Serikali ilikanusha hayo na iliwalaumu waasi kwa mashambulio.
Kila upande unasema haufikiri kuwa upande wa pili unaweza hasa kudhibiti majeshi yake.
Maelfu ya watu wamekufa katika vita hivyo baina ya jeshi la serikali ya Rais Salva Kiir na wanajeshi watiifu kwa naibu wake wa zamani, Riek Machar.
No comments:
Post a Comment