*Chatoa taarifa kuhusu nafasi ya Uwaziri wa Fedha
Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akizungumza na waandishi wa habari, Makao Makuu, Dar es Salaam leo, kuhusu uteuzi wa Raias Jakaya Kikwete wa Baraza la Mawaziri, hususan nafasi ya Uwaziri wa Fedha, iliyokwenda kwa aliyekuwa Naibu Waziri, Saada Salum Mkuya. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Tanzania Bara, Julius Mtatiro na kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa chama hicho, Abdul Kambaya.

Profesa Ibrahim Lipumba akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akizungumza na waandishi wa habari, Makao Makuu, Dar es Salaam leo, kuhusu uteuzi wa Raias Jakaya Kikwete wa Baraza la Mawaziri, hususan nafasi ya Uwaziri wa Fedha, iliyokwenda kwa aliyekuwa Naibu Waziri, Saada Salum Mkuya. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Tanzania Bara, Julius Mtatiro na kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa chama hicho, Abdul Kambaya.
Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Januari 26 2014
WAZIRI WA FEDHA ANATOSHA?
Rais Kikwete amefanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri baada ya Mawaziri
wanne kuachishwa kazi kutokana na kashfa ya uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu
uliotokea katika Operesheni Tokomeza na kifo cha Waziri wa Fedha. Katika
mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, Rais Kikwete hakuzingatia malalamiko ya
Sekretariati ya CCM kuwa Mawaziri Mizigo wanakiathiri chama CCM hususani wakati
huu tukielekea katika uchaguzi mkuu 2015.
Mawaziri walioanishwa na Katibu Mkuu na Katibu Mwenezi wa CCM kuwa ni
mizigo na kuhojiwa na Kamati Kuu ya CCM na ambao wamebaki katika Baraza la
Mawaziri ni pamoja na Dk Shukuru Kawambwa (Elimu), Christopher Chiza (Kilimo),
Dk Abdallah Kigoda (Viwanda), Celina Kombani (Utumishi wa Umma) na Hawa Ghasia
(Tamisemi). Mhe. Saada Mkuya Salum akiwa Naibu Waziri alihojiwa kwa niaba ya
aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa ambaye kwa sasa ni marehemu. Rais
Kikwete amemteua Mhe. Saada Mkuya Salum kuwa Waziri wa Fedha na Uchumi.
Waziri wa Fedha na Uchumi ndiyo msimamizi mkuu wa sera za uchumi za
nchi. Ana majukumu ya kusimamia uandaaji wa bajeti ya serikali ikiwa ni pamoja
na kuandaa miswada ya sera za kodi na kuzitekeleza, kuandaa makadirio ya
matumizi ya serikali na kusimamia utekelezaji wake baada ya kupitishwa na
Bunge. Sera za serikali kupitia wizara ya fedha ni nyezo muhimu ya kukuza
uchumi kwa kuhakikisha kuwa matumizi ya serikali yana tija ya juu, kuongeza
ajira, kuhakikisha sekta za jamii hususan afya na elimu zinatengewa fedha za
kutosha, kudhibiti mfumko wa bei kuhakikisha nchi ina akiba ya kutosha ya fedha
za kigeni, kudhibiti ongezeko la deni la taifa, kuhakikisha idara na mashirika
ya serikali yanawajibika katika matumizi yao ya fedha za umma.
Waziri wa Fedha ndiye anayeongoza majadiliano na mashirika ya kimataifa
yanayohusu sera za uchumi, fedha, misaada na mikopo kama vile Benki ya Dunia,
Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Benki ya Maendeleo ya Afrika, Mashirika ya
Misaada ya Nchi zilizoendelea kama vile DFID (Uingereza), SIDA (Sweden), DANIDA
(Denmark), USAID na MCC (Marekani) na kadhalika.
Tanzania imeanza kukopa katika masoko ya biashara kwa kasi na ari mpya.
Waziri wa Fedha ana wajibika kuweka break nchi isije ikajikuta ina madeni
isiyoweza kuyalipa.
Ndani ya serikali kuna mivutano mikubwa kati ya wizara ya fedha na
wizara, idara na mashirika mengine. Kila wizara inataka itengewe fedha zaidi.
Wizara ya fedha lazima isimamie matumizi yasizidi mapato. Waziri awe na uwezo
wa kupambana na Mawaziri wenzake ambao wanakiuka bajeti zao. Awe na ujasiri wa
kumueleza Rais kwa heshima na taadhima ofisi yake izingatie bajeti
iliyopitishwa. Kuna taarifa kuwa katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha, Ofisi
ya Rais ilitumia zaidi ya bajeti ya mwaka mzima ya safari za Rais. Waziri wa
Fedha anapaswa kumueleza Bosi wake kwamba sote tunawajibika kuheshimu bajeti
iliyopitishwa na Bunge.
Waziri wa
Fedha ndiye kiranja wa asasi nzito kama vile Benki Kuu BOT, Mamlaka ya Mapato
(TRA), Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Amana (Capital Markets and Securities
Authority), Mamlaka ya Usimamizi wa Ununuzi wa Umma (Public Procurement
Regulatory Authority), Idara ya Usimamizi wa Bima (Insurance Supervisory
Department), Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi (National Board of
Accountants and Auditors) na kadhalika.
Wizara ya
Fedha ndiyo inayosimamia hisa za serikali katika kampuni kama vile National
Microfinance Bank (NMB), Tanzania Investment Bank (TIB), National Bank of
Commerce (NBC), Tanzania Postal Bank (TPB), National Insurance Corporation
(NIC) na mashirika mengine ya Umma. Wizara ya Fedha inasimamia mifuko ya
Pensheni ikiwemo Public Service Pension Fund, Parastatal Pension Fund na Government
Employees' Provident Fund.
Waziri wa
Fedha anastahiki kuwa na uelewa na uwezo mkubwa wa kuchambua sera za uchumi,
kujenga hoja wakati wa majadiliano na mashirika ya kimataifa, kuweza kuonyesha
uongozi katika mijadala na mawaziri wenzake na asasi nyeti kama vile Benki Kuu.
Rais Kikwete amemteua Mhe. Saada
Mkuya Salum kuwa Waziri wa Fedha baada ya kifo cha Dr William Mgimwa. Uteuzi wa
mwanamke kuwa Waziri muhimu ni jambo jema katika kupambana na mfumo dume. Mhe.
Saada ni Mzanzibari. Moja ya kero za Muungano ni kuwa Wazanzibari hawapewi
fursa kuongoza wizara muhimu kama vile Wizara ya Fedha. Mhe. Zakhia Meghji
ambaye aliteuliwa na Rais Kikwete baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 alikuwa
mwanamke wa kwanza kuwa Waziri wa Fedha. Haidhuru yeye pia ana asili ya
Zanzibar lakini alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Kilimanjaro.
Kashfa ya uchotaji wa fedha za EPA Benki Kuu ilimlazimisha ajiuzulu. Kumteua
Saada Mkuya Salum kuwa waziri kunaua ndege wawili kwa jiwe moja. Ni mwanamke na
Mzanzibari wa Zanzibar.
Wasifu wa Mhe. Saada Mkuya Salum
uliowekwa katika tovuti ya Bunge unaonesha kwa Mhe.Saada alijiunga na CCM mwaka
2000 na yeye ni mwanachaama wa kawaida. Bi Saada alimaliza kidato cha 6 mwaka
1995 Sekondari ya Lumumba Zanzibar. Shule ya Msingi alisomea Kisiwandui na
sekondari ya kawaida (O level) alisomea Hamamni. Mwaka 1997 – 99 alifanya
masomo ya biashara na akatunukiwa sitashahada ya juu. Kati ya 2000 – 2002
alifanya masomo ya shahada ya pili ya biashara (Courses for the Second Degree
in Business) na akapata cheti (certificate). CV imetaja shule ya msingi
alizosomea lakini vyuo alivyosomea havikutajwa.
Alianza kufanya kazi Hazina
Zanzibar mwaka 2003 kama afisa. Mwaka 2006 alikuwa Afisa Tawala (Administrative
Officer). Kati ya mwaka 2008 na 2010
alisomea shahada ya Master of Finance. Chuo alichosomea hakikuelezwa. Kutotaja
Chuo kunaweka wasiwasi wa ubora wa shahada aliyoipata. Mwaka 2011 aliteuliwa
kuwa Kamishna wa Fedha (Commissioner of Finance) na Mwaka 2012 aliteuliwa kuwa
Naibu Waziri wa Fedha. Baadhi ya Wabunge niliyozumgumza nao wamenieleza kuwa
Mhe. Saada amefanya kazi nzuri Bungeni hasa katika kipindi ambacho Marehemu Dr
Mgimwa alikuwa mgonjwa.
Ikiwa wasifu uliobandikwa katika
tovuti ya Bunge ni sahihi ni wazi Mhe. Mkuya hana uzoefu wa kisiasa, kitaaluma
na kiutawala wa kuongoza Wizara nzito na nyeti. Sina uhakika ana uelewa
wakutosha kuhusu menejimenti ya fedha za umma (Public Financial Management),
upembuzi yakinifu wa miradi ya umma, athari za nakisi ya bajeti katika mfumko
wa bei, deni la taifa na upatikanaji wa mikopo kwenye sekta binafsi. Sera
muhimu ya kukuza na kubadilisha mfumo wa uchumi, hususani kuendeleza viwanda
vya ndani, kuongeza uuzaji wa bidhaa nchi za nje na hivyo kuongeza ajira ni
kuwa na thamani halisi ya sarafu (real exchange rate) yenye kuongeza ushindani
katika soko la dunia. Kuongezeka kwa tija na ufanisi katika uzalishaji bila
kubadili thamani ya shilingi kunaongeza ushindani wa bidhaa za Tanzania katika
soko la dunia. Mfumko wa bei unapunguza ushindani wa bidhaa za Tanzania ndani
ya nchi na kwenye soko la dunia na hivyo kuathiri ongezeka la ajira. Sera za
riba na upatikanaji wa mikopo ni suala muhimu katika kuendeleza uwekezaji ambao
utakuza uchumi na kuongeza ajira.
Serikali inakabiliwa na matatizo
makubwa ya fedha. Matumizi yanaongezeka kwa kasi kubwa kuliko mapato. Bajeti
inayowasilishwa na serikali Bungeni imekuwa na makadirio makubwa ya mapato
kuliko ukusanyaji halisi. Matumizi ya kawaida yanaongezeka kwa kasi kubwa na
kupunguza uwezo wa serikali kuchangia katika Bajeti ya Maendeleo.
Nakisi ya bajeti imeongezeka toka shilingi
bilioni 389 mwaka wa 2007/08 sawa na asilimia 1.7 ya pato la taifa na kufikia
shilingi bilioni 2992 mwaka 2012/13 sawa na asilimia 6.2 ya pato la taifa.
Mwaka huu wa fedha 2013/14, bajeti imeishafumka. Mapato ni madogo kuliko makadirio.
Matumizi ni makubwa. Serikali inalimbikiza madeni kwa makampuni yanayoiuzia
bidhaa na huduma.
Serikali imekuwa inakopa katika
masoko ya kibiashara kwa gharama kubwa na deni la taifa linaongezeka kwa kasi.
Deni la taifa limeongezeka toka shilingi trilioni 5.9 mwaka 2007 sawa na
asilimia 28.4 ya pato la taifa na kufikia shilingi trilioni 22 mwaka 2013 sawa
na asilimia 42.5 ya pato la taifa. Tukiendelea na kasi hii ya kukopa Rais
Kikwete ataiachia nchi tatizo kubwa la deni la taifa na hasa deni la nje.
Katika sekta ya ujenzi wa
barabara kuna tatizo kubwa la makandarasi wengi kutolipwa kwa wakati na hivyo
kucheleweshwa kukamilishwa kwa miradi. Wakati mwingine Wizara ya Ujenzi inatia
sahihi miradi mipya hata kama hakuna fedha zilizotengwa ndani ya bajeti. Waziri
wa Fedha ana wajibu wakuweka nidhamu katika matumizi ya serikali. Awe na uwezo
wa kumueleza Waziri Magufuli asiweke sahihi miradi mipya ya barabara ambayo
haijatengewa fedha.
Uendeshaji wa TANESCO una gharama
kubwa katika bajeti ya serikali. Tanesco ilipata hasara ya dola milioni 240 na
ina limbikizo ya madeni ya dola milioni 276
Katika kipindi hiki tuna mchakato
wa katiba mpya ambao una gharama zake. Bunge la Katiba litaanza kukutana mwezi
Februari. Bunge litafuatiwa na Bunge la Bajeti. Tume ya Uchaguzi inawajibika
kuboresha Daftari la Wapiga kura kabla ya kura ya maoni. Tume haijaboresha
daftari kwa sababu ya kukosa fedha. Uandikishaji wa vitambulisho vya taifa
unasuasua kwa kutokuwa na fedha za kutosha.
Katika kipindi cha kueleka
uchaguzi mkuu nidhamu ya matumizi ya serikali inatoweka. Rais na wapambe wake
wanafikiria taratibu za maisha baada ya kuondoka Ikulu. Kuna kuwa na shinikizo
kubwa za misamaha ya kodi na mikataba inayoweza kuwanufaisha katika kipindi cha
kustaafu. Kuna shinikizo ya kupata fedha za kusaidia Chama Tawala wakati wa
uchaguzi. Katika kipindi cha pili cha Rais Mkapa akielekea kun’gatuka aliuza
nyumba za serikali kwa bei poa kwa mawaziri, viongozi wa CCM na watumishi wa
serikali. Kashfa ya kuchota fedha za EPA ilitokea wakati tukielekea uchaguzi wa
2005. Waziri wa Fedha anawajibika kupambana na shinikizo hizo.
Baada ya kuchaguliwa kuwa Rais
mwaka 2005, Mhe. Kikwete alieleza kuwa hakuna Chuo kinachofundisha Uwaziri kwa
hiyo yeyote anaweza kuwa Waziri. Bila shaka mtazamo huu unachangia kuteua
Mawaziri Mizigo wasiyokuwa na sifa au uwezo wa kutekeleza majukumu yao. Chanzo
cha tatizo siyo Mawaziri Mizigo bali ni Rais Mzigo anayetokana na Chama mzigo.
Watanzania tunakabiliwa na
matatizo ya gharama kubwa za maisha, ukosefu wa ajira, elimu duni, huduma mbovu
za afya, kukithiri kwa rushwa na utawala mbovu. Tunapaswa kujipanga kukiondo
Chama Mzigo madarakani.Mawaziri mizigo wanatokana na raisi mizigo na raisi
mizigo wanatokana na chama mizigo.
Prof. Ibrahim Haruna Lipumba
Mwenyekiti
No comments:
Post a Comment