TANGAZO


Friday, January 10, 2014

Abiria wa treni waliokwama wakiwa tayari kusafirishwa kwa mabasi

Abiria ambao walikwama kusafafiri na Treni ya Kati, wakiwa hawajui la kufanya kutokana na kukosa chakula katika stesheni ya Reli ya mjini Dodoma walipotangaziwa kuanza kusafirishwa kwa mabasi lakini mpaka kufikia leo jioni zaidi ya abiria 900 walikuwa bado hawapatiwa usafiri huo.
Abiria akipata mlo pamoja na watoto wake katika Stesheni ya Reli ya Dodoma leo. Zaidi ya abiria 900 walikuwa bado hawajapatiwa usafiri hadi jioni ya leo
Abiria waliokwa na treni wakiwa Stesheni ya Dodoma leo, wakusubiri mabasi kwa ajili ya safiri wa kuelekea Mikoa ya Morogoro na Dar es saalam ambapo Shirika la Reli limewakodia mabasi kutokana na kushindwa kuendelea na safari kutokana na Mafuriko maeneo ya Gulwe na Godegode, wilayani Mpwapwa Dodoma.
Mfanyakazi wa Shirika Reli, Kituo cha Dodoma akiandika tangazo
katika ubao wa matangazo, lililowataka abiria wa kuelekea Mikoa
ya Kanda ya Ziwa kurudishiwa nauli zao kutokana na usafiri wa treni kusitishwa kwa muda usiojulikana.
Askari wa kuzuia Ghasia (FFU), wakiangalia usalama kwa abiria wa treni waliokwama kuendelea na safari yao kutokana na treni kushindwa kuendelea na safari tangu jana mara baada ya kufika kituo cha Relwe cha Dodoma kutokana na maji ya mvua kufunika reli, wilayani Mpwapwa.
Abiria ambao walikwama kusafafiri na Treni ya Kati, wakiwa hawajui la kufanya kutokana na kukosa chakula katika stesheni ya Reli ya mjini Dodoma walipotangaziwa kuanza kusafirishwa kwa mabasi laki mpaka kufikia leo jioni zaidi ya abiria 900 walikuwa bado hawapatiwa usafiri huo.

Na John Banda, Dodoma
SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limelazimika kuwapakia kwenye
mabasi abiria wake waliokwama kwa siku mbili katika Stesheni ya
kituo cha Dodoma kwa kutumia usafiri wa Treni kutokana na
kushindikana kwa ukarabati  unaofanyika mpaka sasa ambao
umeonekana kushindikana kutokana na wingi wa maji ulipo
kwenye eneo hilo la Gulwe na Godegode lililopo wilayani
Mpwapwa, Mkoa wa Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Stesheni Masta wa Kituo cha Reli Dodoma Zakaria Kilombele alisema kuwa kutokana na hali hiyo ya ukarabati huo unaoendela kwa hivi sasa kwenye njia hiyo ya reli shirika limeamua kuwasafisha abiria hao waliokwama kwa kutumia mabasi.

Kilombele alisema abiria hao waliokwama kwa siku mbili toka
wafike kutoka mikoa ya Kigoma, Tabora  na Singida na Mwanza
mkoani hapa, jumla yao wamefikia 1800 na Shirika limewakodishia mabasi yapatayo 24, mpaka kufikia leo (jana jioni) abiria wote watakuwa wamesafirishwa na mabasi hayo yaliyokondishwa na shirika.

“Mpaka sasa tayari abiria wapatao 935 wameshaondoka na
ninategemea hawa wengine waliobaki mpaka kufikia leo jioni (jana
jioni) ni matarajio yangu watakuwa wamesafirishwa,kwa kuwa
ninategemea kuletewa mabasi yapatayo tisa “alisema Kilombele.

Akizungumza kuhusu ukarabati unaoendelea kwenye eneo hilo
korofi la Gulwe na Godegode alisema mpaka juzi alasili hali ilikuwa nzuri na tuliruhusu gari la abiria kuendelea na safari,lakini ilipofika majira ya saa 12 jioni maji yalianza kujaa kwenye eneo hilo na tukakalazimika abiria hao kurudishwa stesheni ya  Dodoma mjini.

Hata hivyo wakizungumza  baadhi ya abiria hao walidai kuwa
shirika hilo kitendo cha kuendelea kuwachelewesha juu ya safari
kuna hatari ya kuwepo mlipuko wa magonjwa matumbo kutokana
na abiria walio wengi kujisaidia hovyo na kusababisha kila sehemu
kuwa na vinyesi.

Mawazo Elisha alisema kwa siku mbili tulizokaa hapo stesheni
karibu abiria wengi wamekuwa wanajisaidia kwenye mabehewa ya
abiria ambayo yamekwama hapo stesheni nay ale mabovu hali hiyo
inatokana vyoo vilivyopo kujaa.

“Vyoo vilivyopo vyote vimejaa na tunalazimika abiria kujisaidia
kwenye mabehewa ambapo uchafu huu umetapakaa kwenye
mataruma ya reli, hali ambayo imekuwa ikileta harufu kali katika
eneo hilo”alisema Mawazo.

Naye Joshua Lazaro alisema shirika kuendelea kuwaweka katika
eneo hilo limesababisha biashara zao kama vile samaki wameanza
kuharibika na kuanza kutoa harufu na wadudu wa aina ya vuza.
Alisema miongoni mwa abiria wana wamesafirisha biashara zao

kama hao samaki na dangaa kwa maana hiyo hivi sasa wameanza
kuharibika na kutuletea hasara kubwa ambayo hatufahamu nani
watahusika.

Hata hivyo abiria walikwisha kata tiketi kuelekea mkoa ya kanda ya ziwa walitangaziwa kurudishiwa nauli zao kutokana na
mkanganyiko huo wa usafiri kwa njia hiyo ya reli uliojitokeza na
mkuu huyo wa stesheni mkoa alisema hakutakuwepo na usafiri kwa
muda usiojuilikana.

Mapema wiki hii jumla ya abiria wapatao 1600 waliokuwa
wametoka mikoa ya Kigoma,Tabora Mwanza na Singina waliokuwa wamesafiri kwa usafiri wa reli walikwama stesheni ya Dodoma mjini na kuwalazimu kufanya maandamano hadi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Rehema Nchimbi kwa lengo la kutaka kuwapatia usafiri mwingine.

No comments:

Post a Comment