Thursday, January 9, 2014
Abiria wa Treni wakwama kuendelea na safari kutokana na mafuriko maeneo ya Gulwe na Mzaganza, Dodoma
Abiria waliokuwa wakisafiri na Treni ya Kati, kuanzia Kigoma kwenda Dar es Salaam wakielekea kwenye Ofisi ya Mkuu wa Stesheni ya Dodoma mara baada ya treni hiyo, kukwama kuondoka kwa sababu ya mafuriko yaliyosababishwa na mvua maeneo ya Gulwe na Mzaganza. (Picha zote na John Banda)
Wasafiri wa treni toka Kigoma na Mwanza kuelekea Morogoro na Dar es Salaam wakiwa wamelala kwenye mabehewa bila kujua cha kufanya baada ya treni hiyo kushindwa kuondoka Dodoma kutokana na Maji kujaa kwenye njia ya reli, maeneo ya Gulwe na Mzaganza.
Abiria hao wakiwa kwenye foleni wakati Mkuu wa Stesheni ya Dodoma, Zacharia Kilombele, ambako walikwama na kushindwa kuondoka, kutoa sh. 3500 za kijikimu kwa kila abiria, wapatao 1600 waliokwama kutokana na mafuriko.
Abiria hao wakiwa kwenye foleni ya kuchua fedha hizo za kujikimu kutoka kwa Mkuu wa stesheni ya Dodoma, Zacharia Kilombele.
Abiria wakiwa wamesongamana dirishani kwa ajili ya kupokea fedha za kujikimu sh. 3500, zilizotolewa na shirika la Reli baada kukwama kuondoka Dodoma leo.
Abiria hao wakiwa kwenye foleni hiyo.
Abiria wa treni iliyokwama Dodoma, wakiwa na watoto wao wakipata chochote wakati wakisubiri hatima yao, huku katika stesheni hiyo kukiwa hakutamaniki kwa uchafu unaotishia afya zao kutokana na abiria zaidi ya 1500 kutakiwa kutumia matundu manne ya vyoo.
Abiri wakiwa wamejipumzisha kwenye viti vya treni hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment