Maafisa wakuu nchini Misri wamesifu sana idadi kubwa ya watu
waliojitokeza kupigia kura ya maamuzi katiba mpya.
Jeshi limekuwa likiwashawishi watu kupiga kura ya ndio ili kuhalalisha
kuondolewa mamlakani kwa aliyekuwa Rais Mohammed Morsi.Siku ya pili ya kura hiyo ambayo ilikuwa Jumatano ilikamilika kwa Amani .
Watu tisa waliuawa Jumanne kwenye mapigano kati ya makundi mawili hasimu yakiwahusisha wafuasi wa Morsi.
Polisi waliwakamata watu 400 katika siku mbili za kwanza za kura hiyo ambao walidaiwa kusababisha vurugu wakati wa shughuli hiyo.
Afisaa mmoja mkuu katika wizara ya mambo ya ndani, alinukuliwa akisema huenda idadi hiyo ilifika asilimia 55 ya wapiga kura.
Matokeo ya mapema yanaonyesha kuwa katiba hiyo imekubalika kwa asilimia 95.
Hata hivyo, wanachama wa vuguvugu la Muslim Brotherhood walisusia kura hiyo.Matokeo ya kura hiyo huenda yakatolewa Ijumaa.
No comments:
Post a Comment