Meli ya Australia imo njiani kuelekea Mashariki wa Antarctica
kwa ajili ya kukwamua meli ya wanasayansi iliyokwama kwenye theluji tangu siku
ya jumanne.
Awali juhudi za uokoaji zilifanywa na wavuja theluji wa Uchina na Ufaransa
lakini walikwama kutokana na unene wa theluji.Wanasayansi wapatao sabini na nne, watalii na wafanyakazi wa meli wapo kwenye meli hiyo iliyokwama inayoitwa .
Meli hiyo imekuwa ikitumiwa na taasisi ya Australasian Antarctic Expedition kufuatilia njia mtafiti Douglas Mawson aliyesafiri kwenye njia hiyo karne iliyopita.
Shokalskiy imejaa chakula cha kutosha na hakuna hatari hii ni kwa mujibu wa timu ya uokoaji.
Pamoja na kunasa, wanasayansi wanaendelea na majaribio ya kisayansi, kupima nyuzi joto kuzunguka theluji iliyoanza kupasuka.
Mamlaka ya Usalama wa Majini ya Australia ambayo ndio inayoratibu uokoaji imesema kikosi cha uokoaji cha Aurora Australis kilitarajiwa kuwasili katika eneo meli hiyo iliponasa siku ya jumapili majira ya saa 9 kwa saa za Afrika Mashariki.
Mitambo mikubwa ya kukata theluji ina uwezo wa kukata theluji yenye unene wa mita 1.6 na uwezo wa kuzoa theluji ya ukuta wa mita tatu kuzunguka eneo la Shokalskiy.
Kama operesheni hiyo ya uokaji itashindikana itabidi helkopa zitumike kuwaokoa.
No comments:
Post a Comment