TANGAZO


Friday, December 6, 2013

Yanayojiri Afrika Kusini

 

Wananchi wamejitokeza katika sehemu nyingi za Afrika Kusini wakiomboleza kifo cha kiongozi wao Mandela


Mandela alisfika sana duniani kote kama mpigania demokrasia
Wananchi wamejitokeza katika sehemu nyingi za Afrika Kusini wakiomboleza kifo cha kiongozi wao Mandela.
Mji wa Johannesburg umemiminika watu waliojitokeza kumkumbuka Mandela na kutoa rambi rambi zao kwa jamii, familia na marafiki wao.
Viongozi duniani pia wameendelea kutuma rambirambi zao kufuatia kifo cha Mandela.
Kifo cha Mandela kilitangazwa hapo jana Alhamisi saa za usiku naye Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma aliyesema kuwa Afrika Kusini inaomboleza kumpoteza kiongozi huyo waliyemuenzi sana kama mtoto wao , baba yao na kiongozi wa taifa hilo.
Je uko Afrika Kusini? Unaweza kututumia picha au video kuhusu yanayojiri huko na tutayaweka hapa kwenye mtandao wetu. Tutumie picha au ujumbe wako wowote kupitia ukurasa wetu wa Bofya FacebookBofya bbcswahili
Mandela alifariki nyumbani kwake mjini Johanesburg na alikuwa ameugua homa ya mapau kwa muda mrefu.
Na wewe pia unaweza kutuma ujumbe wako kupitia ukurasa wetu wa Bofya Facebook ambao kisha nitauweka kwenye mtandao wa Bofya bbcswahili
Ingia kwenye ukurasa wetu waBofya facebook Bofya Bofya facebook uweke ujumbe wako

14:30 pm Rais wa Uganda Yoweri Museveni
Mzee Mandela, miongonimwa wengine kama Oliver Tambo, Govan Mbeki na wengine, walijitlea maisha yao na ujana wao wote katika kupigania haki na kuikomboa Afrika Kusini. Walijivunia kweli walichoamini na wakatekeleza. Sasa ni jukumu letu na wadogo wetu kuendeleza kazi ya Mandela.

Lohay Langay Mayo Wa Gallapo. Kama Nchi Iliyoongoza Mapambano Ya Ukombozi Kusini Mwa Africa, Imekuwa Ni Jambo Jema Kutangaza Maombolezo Kwa Siku Tatu. Poleni Wananchi Wa Africa Kwa Ujumla

13:32pm: Rais wa Malawi Joyce Banda, "Wakati kama huu, sote tumepata mshtuko. Sio kuwa hatukujua kitatokea, lakini ni huzuni kwa tulichopoteza. Ningependa kuelezea masikitiko yangu kwa kumpoteza kijana wa Afrika Dr. Nelson Mandela kwasababu vita alivyopigana sio tu dhidi ya ubaguzi wa rangi bali ni vita dhidi ya unyanyasaji wa aina yoyote dhidi ya binadamu. Na ndio maana vijana, na wazee, wake kwa waume, weupe na weusi tajiri na masikini wote wamejihusisha na yeye na vitu alivyopigania."

Lohay Langay Mayo Wa Gallapo, asema kupitia Bofya facebook Kama Nchi Iliyoongoza Mapambano Ya Ukombozi Kusini Mwa Africa, Imekuwa Ni Jambo Jema Kutangaza Maombolezo Kwa Siku Tatu. Poleni Wananchi Wa Africa Kwa Ujumla

14:17 pm :Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema kuwa Hayati Nelson Mandela atazikwa tarehe kumi na tano Jumapili mwezi Disemba katika eneo la Qunu mkoa wa Estern Cape.

13:10 pm: Waziri mkuu wa India, Manmohan Singh, "Kifo cha mandela. Huyu alikuwa mwakilishi wa utu duniani. Pia amekuwa chanzo cha matumaini kwa wengine wengi ambao wanakabiliana na unyanyasaji na kunyimwa haki, hata miaka yote hiyo baada ya kuwakomboa watu wake wenyewe. Katika ulimwengu uliogubikwa na migawanyiko, amekuwa mfano mwema wa utangamano na sioni uwezekano wa kupatikana mwingine kama yeye katika miaka mingi ijayo."

11:00 am:Bofya Charles Charlloh Yabuna wa Kakamega, Kenya anasema kupitia Bofya Facebook kua Wafrika kwa jumla tunaomboleza kifo cha mzalendo wetu

10:57 am : Bofya Ahamba Bokyo yupo Durban na kupitia Bofya Facebook anasema maombolezi yanaendelea salama kila mtu yuko kimia na machungu moyoni

10:40 AM: Bofya Adili Mwasomola kwenye ukurasa wake waFacebookamesema >natokea Kurasini DSMd TZ "katika afrika MANDELA ni mmoja wa viongozi walioifanya AFRIKA isiwe nyeusi TENA bali iwe sehemu salama kwa kuishi kila mtu bila kuwepo ubaguzi..... APUMZIKE KWA AMNI YOOOTE.... MBELE YAKE NYUMA YAKE

10:35 am: Bofya Ulimboka Lugano kupitia ukurasa wake wa Bofya Facebook anasema ameanza kumsikia Mandela akiwa anamalizia uongozi wake, na alitarajia kua Mandela angekaa madarakani kama rais kwa muda mrefu lakini kumbe nia yake haikuwa kuongoza bali kumkomboa mwana Afrika kusini kutoka katika ubaguzi wa rangi, namkumbuka kwa kitendo hicho cha kipekee, pia namkumbuka kupitia kusoma kwa roho yake isiyo kata tamaa pamoja na ugumu na kukosekana kwa uhuru wa mtu mweusi kutoka kwa serikali ya makaburu aliweze kuimarisha jeshi lake la 'Umkontho we sizwe'.

No comments:

Post a Comment