Vurugu zimezidi kusambaa katika maeneo mbali mbali nchini
Jamuhuri ya Afrika ya Kati.
Wapiganaji wa kundi la Seleka wanalaumiwa kuendesha mfululizo wa mashambulizi
dhidi ya wakristo ambapo katika kijiji kimoja watu watano wanaripotiwa
kuuawa.Mwandishi wa habari wa BBC katika mji mkuu wa Bangui anasema mamia ya vijiji vipi chini ya himaya ya wapiganaji na kusababisha raia kujificha kwenye misitu. Raia hao sasa wanaomba jamii ya kimataifa kuingilia kati.
Kikosi kidogo cha majeshi ya Umoja wa Afrika wa kulinda amani nchini humo kinasubiri kuengezewa nguvu na majeshi ya Ufaransa ambayo inatarajiwa kutuma askari zaidi.
Kufuatia hali ilivyo nchini humo kwa sasa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa litarajiwa kukutana kujadili suala hilo siku ya Alhamisi.
No comments:
Post a Comment