TANGAZO


Monday, December 23, 2013

UN: Hatutawaacha raia Sudan Kusini

 


Kikosi cha Umoja wa Maifa Sudan Kusini

Kikosi cha Umoja wa Mataifa kilichopo Sudan Kusini kimesema hawatawaacha raia baada ya wiki ya mapigano ya kikabila yaliyoibuka na kusababisha hofu kwa raia.
 
Msemeji Kikosi cha Umoja wa Mataifa aliyepo Juba Joseph Contreras ameiambia BBC kuwa katika maeneo ya Umoja wa Mataifa ambapo kuna wakimbizi zaidi elfu ishirini wapo salama.

 
Hata hivyo amesema Umoja wa Mataifa umeshindwa kusambaza chakula katika mji huo.
Wakati huo huo Maafisa wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini wamesema hali nchini humo ni ya wasi wasi kutokana na mapigano yanayozidi kusambaa nchini humo.

Mratibu wa mashirika ya misaada Toby Lanzer ameiambia BBC kuhusu mauaji katika mji Bor, katika jimbo la Jonglei ambalo lipo mikononi mwa waasi.

Kikosi cha Umoja wa Mataifa kilichopo Sudan Kusini ametaka viongozi wa kisiasa wa pande zinazopingana kukubaliana na kuanzisha mazungumzo.

Mapigano yalizuka kati ya wapiganaji wanamuunga mkono Rais Salva Kiir na wale wanaomuunga mkono Makamu wa Rais wa zamani takriban wiki moja iliyopita.

Wakati huo Marekani imesema itawaondoa raia wake waliopo katika eneo la Bor.

Wamarekani wanne wafanyakazi wa huduma walijeruhiwa siku ya jumamosi wakati ndege waliyokuwa wakisafiria iliposhambulia, na kuchelewesha juhudi za uokoaji jambo lililofanya Rais wa Marekani Barak Obama kufikiria hatua nyingine za kuchukua.

No comments:

Post a Comment