TANGAZO


Sunday, December 22, 2013

Treni yaumiza watu Kibera, Nairobi

 

Nyumba za Kibera zimejengwa karibu sana na njia ya reli
Waokozi wana wasiwasi kuwa pengine watu kadha wamenasa chini ya treni iliyopinduka katika mitaa ya Kibera, Nairobi - eneo la watu maskini.
Watu kama saba walijeruhiwa wakati mabehewa mane ya mizigo yalipopinduka juu ya nyumba kando ya njia ya reli.

Treni ya abiria imefikwa na ajali mjini Nairobi, katika mitaa ya maskini.
Waokozi wanajaribu kutafuta nafasi katika mtaa wenye nyumba zilizogandana sana, ili kuleta mashini ya kunyanyua mabehewa ili kuwafikia wale walionasa.
Mabehewa yalianguka juu ya nyumba zilizo karibu na njia ya reli.
Magazeti yanaarifu kuwa kazi za uokozi zimezingika kwa sababu watu wengi wamezonga eneo hilo.

No comments:

Post a Comment