Huku bunge la afrika kusini likifanya kikao maalum cha
kumheshimu mandela ,mwanawe mkubwa wa kike Makaziwe ameiambia BBC kuhusu siku za
mwisho za maisha ya babaake.
Amesema kuwa ijapokuwa hakuwa akifungua macho mara kwa mara,alikuwa na
uhakika kuwa aliweza kusikia vile familia yake ilivyompenda.Makaziwe amekiri kuwa hakuweza kuwasiliana vyema sana na babake na kwamba babaake hakuweza kuonyesha hisia zake,lakini yote hayo alitaka familia yake kupatana.
Amesema kitu kikubwa alichoelimishwa na babaake ni kuwa na ujasiri wa kusamehe.
No comments:
Post a Comment