TANGAZO


Friday, December 27, 2013

Rais Kikwete arejea nchini, aenda Muhimbili kuwajulia wagonjwa



Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal akimlaki Rais Jakaya Kikwete, muda mfupi baada ya kuwasili nchini akitokea jijini New York, Marekani ambapo alikwenda kwa ukaguzi wa kawaida wa afya yake. Akiwa nchini humo,  Rais Kikwete alialikwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon na kufanya naye mazungumzo kuhusu ushiriki wa majeshi ya Tanzania katika ulinzi wa Amani katika nchi mbalimbali. (Picha zote na Freddy Maro)


Rais Jakaya Kikwete, akizungumza na Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, muda mfupi baada ya kuwasili nchini akitokea jijini New York, Marekani ambapo alikwenda kwa ukaguzi wa kawaida wa afya yake.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali mtoto Andrew Simba(15) aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati Rais alipowatembelea na kuwafariji  baadhi ya wagonjwa katika wodi ya Mwaisela leo. (Picha zote na Freddy Maro).
 

No comments:

Post a Comment