TANGAZO


Wednesday, December 11, 2013

Postamasta Mkuu, Deos Mndeme atoa mpango kabambe wa miaka 10 wa Shirika la Posta



*Shirika lakusanya shilingi bilioni 44.5 kufika mwaka 2012

Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deos Mndeme, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu malengo waliyojiwekea katika kulifikisha shirika hilo katika viwango vya juu vya mafanikio kiutendaji. Kulia ni Meneja Mkuu wa TPC, Fortunatus Kapinga na katikati ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari, Maelezo, Zamaradi Kawawa.
Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deos Mndeme (katikati), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu malengo waliyojiwekea katika kulifikisha shirika hilo katika viwango vya juu vya mafanikio kiutendaji. Kushoto ni Meneja Mkazi wa shirika hilo, Zanzibar, Mwanaisha Ali Saidi na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari, Maelezo, Zamaradi Kawawa.
Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deos Mndeme, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu malengo waliyojiwekea katika kulifikisha shirika hilo, katika viwango vya juu vya mafanikio kiutendaji. Kushoto ni Meneja Mkazi wa shirika hilo, Zanzibar, Mwanaisha Ali Saidi na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari, Maelezo, Zamaradi Kawawa.
Baadhi ya Mameneja wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakimsikiliza Postamasta Mkuu, Deos Mndeme (hayupo pichani), wakati alipokuwa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu malengo waliyojiwekea katika kulifikisha shirika hilo katika viwango vya juu vya mafanikio kiutendaji.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakimsikiliza Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deos Mndeme (hayupo pichani), wakati alipokuwa akifafanua jambo kuhusu malengo waliyojiwekea katika kulifikisha shirika hilo katika viwango vya juu vya mafanikio kiutendaji.
Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deos Mndeme (kulia), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu malengo waliyojiwekea katika kulifikisha shirika hilo katika viwango vya juu vya mafanikio kiutendaji.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakichukua maelezo yaliyokua yakitolewa na Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deos Mndeme, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, wakati alipokuwa akielezea kuhusu malengo waliyojiwekea katika kulifikisha shirika hilo katika viwango vya juu vya mafanikio kiutendaji.
Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deos Mndeme, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu malengo waliyojiwekea katika kulifikisha shirika hilo katika viwango vya juu vya mafanikio kiutendaji. Kushoto ni Meneja Mkazi wa shirika hilo, Zanzibar, Mwanaisha Ali Saidi.
Baadhi ya wakuu wa Shirika la Tanzania (TPC), wakimsikiliza Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deos Mndeme, (hayupo pichani), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu kulifikisha shirika hilo katika viwango vya juu vya mafanikio kiutendaji.
Waandishi wa habari, wakimsikiliza Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deos Mndeme, wakati alipokuwa akifafanua jambo katika mkutano huo, Idara ya Habari, Maelezo, Dar es Salaam leo.
Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deos Mndeme, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akizungumza nao kuhusu malengo waliyojiwekea katika kulifikisha shirika hilo katika viwango vya juu vya mafanikio kiutendaji. Kushoto ni Meneja Mkazi wa shirika hilo, Zanzibar, Mwanaisha Ali Saidi na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari, Maelezo, Zamaradi Kawawa.
Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deos Mndeme, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, wakati wa mkutano huo leo. Kushoto ni Meneja Mkazi wa shirika hilo, Zanzibar, Mwanaisha Ali Saidi na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari, Maelezo, Zamaradi Kawawa.
Meneja wa Barua na Logistiki wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fadya Zam, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati wa mkutano huo, jijini leo.
Meneja Mkuu Uendeshaji wa Biashara wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga akielezea kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya matumizi ya TEHAMA katika Ofisi za Shirika, zipatazo 86 hapa nchini ili kutoa huduma kwa ufanisi.
Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta nchini, Deus Mndeme akielezea kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya mpango kabambe wa miaka 10 wa shirika hilo kupitia utekelezaji wa sera na mipango mbalimbali pamoja na dira ya maendeleo ya Taifa ya 2025, kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari, Maelezo,  Zamaradi Kawawa.
 

Baadhi ya waandishi wa habari wakimfuatilia kwa karibu Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Deos Mndeme wakati akielezea mpango kabambe wa miaka 10 wa shirika hilo kupitia utekelezaji wa sera na mipango mbalimbali pamoja na dira ya maendeleo ya Taifa ya 2025.
 


Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta nchini, Deos Mndeme akielezea kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya mpango kabambe wa miaka 10 wa shirika hilo kupitia utekelezaji wa sera na mipango mbalimbali pamoja na dira ya maendeleo ya Taifa ya 2025, Kushoto ni Meneja Mkazi wa Shirika la Posta, Zanzibar, Mwanaisha Ali Said. (Picha zote na Eliphace Marwa)
 




Na Frank Mvungi
SHIRIKA la Posta Tanzania limefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi Bilioni 44.5 kufikia mwaka 2012 ikiwa ni matokeo ya kuboreshwa kwa huduma zake hapa nchini.
 
Hayo yamesemwa na Posta Masta Mkuu Bw. Deos Mndeme wakati alizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu mafaniko yaliyofikiwa na shirika hilo tangu kuanzishwa kwake.
 
Mndeme amesema kuwa mafanikio hayo yametokana na huduma bora zenye hadhi ya kimataifa zinazotolewa na shirika hilo kwa wananchi hali itakayosaidia kuongeza mapato ya Serikali.
 

“Shirika limejipanga zaidi kutumia TEHAMA katika kuboresha huduma zake ikiwa ni moja ya mkakati utakaosaidia serikali kuongeza mapato na kufikia malengo ya muda mrefu yaliyowekwa na shirika pia tumejipanga kuendelea kuboresha huduma tunazozitoa ili kuendana na mahitaji ya wakati” alisema Mndeme.
 
Mndeme aliongeza kuwa kwa sasa shirika limeunganisha Ofisi 86 kwenye Wilaya na Miji kote nchini na mfumo wa mawasiliano ili kuongeza idadi ya wateja wanaohudumiwa,kuondoa ucheleweshaji na kuondoa  malalamiko ya wateja.
 
Katika kuhakikisha shirika linashiriki kikamilifu katika shughuli za kitaifa Mndeme alisema shirika litafanya uzinduzi wa toleo jipya la stempu ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika sherehe hizo zitakazofanyika Disemba 28 mwaka huu.  

Shirika la Posta ni mwanachama wa Umoja wa Posta Duniani (UPU) ambalo Tanzania ilijiunga mwaka 1963 na kwa hivi sasa idadi ya nchi wanachama wa umoja huo ni 192 malengo ya Umoja huo ni pamoja na kuisimamia,utumiaji wa barua,Vipeto,Vifurushi katika nchi mbalimbali duniani, kutoa  ushauri, usuluhishi, kuunganisha ushirikiano baina ya nchi wanachama na kutoa misaada ya kiufundi.

 

 
 
 
 

No comments:

Post a Comment