Wezi wamevunja na kuingia nyumbani kwa Askofu mstaafu Desmond
Tutu.
Polisi wamesema wizi huo ulifanyika wakati bwana Tutu akiwa katika ibada ya
Nelson Mandela Mjini Johannesberg.Aidha wameelezea kuwa uvamizi ulifanyika nyumbani kwake mjini Cape Town Ahamisi jioni baada ya kutoa hotuba katika ibada ya Mandela siku hiyo.
Ibada hiyo ilifanyika katika uwanja wa FNB mtaani Soweto.
Wizi na uvamizi wa nyumba za watu ni jambo la kawaida nchini Afrika Kusini ambako visa vya uhalifu viko juu sana.
No comments:
Post a Comment