TANGAZO


Sunday, December 22, 2013

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki azindua Kitabu cha Mwongozo wa Kuwasaidia Wanawake waliofanyiwa ukatili, kilichoandaliwa na WLAC

 
 Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angellah Kairuki (katikati), Mwenyekiti wa Bodi wa Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake na Watoto (WLAC),Nakazael Tenga (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho,Theodosia Muhulo, wakionesha Kijitabu cha mwongozo wa kuwasidia wanawake waliofanyiwa ukatili, baada ya kukizindua rasmi Dar es Salaam jana.
 Wadau wakiwa kwenye uzinduzi huo.


 Naibu Waziri Kairuki akikaribishwa baada ya kuwasili Makao Makuu ya WLAC
 Naibu Waziri Kairuki (kushoto), akiteta jambo na
Mwenyekiti wa Bodi wa Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake na Watoto (WLAC),Nakazael Tenga
 Wadau na wanahabari wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa WLAC, Theodosia Muhulo (kushoto), akitoa neno la kuwakaribisha wageni.
 Mwenyekiti wa Bodi wa Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake na Watoto (WLAC),Nakazael Tenga, akihutubia kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi wa uzinduzi huo, Waziri Kairuki.
 Waziri Kairuki akihutubia katika uzinduzi huo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa WLAC, Theodosia Muhulo (kushoto),akimuelekeza jambo Waziri Kairuki katika maktaba ya kituo hicho.
 Maofisa wa WLAC wakiwa kwenye hafla hiyo
 Waziri Kairuki akipokea zawadi ya machapisho mbalimbali yahusuyo ukatili wa kijinsia.

Na Dotto Mwaibale

KITUO cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake na Watoto (WLAC), kimeiomba serikali kuanzishwe kwa Mahakama ya kifamilia kwa ajili ya kuongeza kasi ya kumaliza haraka kesi za ukatili wa kijinsia nchini.

Ombi hilo lilitolewa na Mwenyekiti wa Bodi wa WLAC, Nakazael Tenga wakati akisoma taarifa ya kituo hicho mbele ya mgeni rasmi Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angellah Kairuki kwenye hafla ya uzinduzi wa Kijitabu cha Mwongozo wa Kuwasaidia Wanawake waliofanyiwa ukatili kilichoandaliwa na WLAC Makao Makuu ya kituo hicho Kinondoni Dar es Salaam leo.

"Pamoja na jitihada tunazozifanya za kuhakikisha ukatili wa jinsia unakomeshwa kwa kushirikiana na taasisi zingine bado tunachanga moto ya kesi za matukio hayo kuchelewa kusikilizwa hivyo ombi letu kwa serikali na wahusika ianzishwe Mahakama ya Familia itakayokuwa ikisikiliza kesi hizo" alisema Tenga.

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Angellah Kairuki alisema badala ya kuanzishwa kwa mahakama hiyo serikali imeanzisha utaratibu wa kusikiliza mashauri hayo kupitia kamati maalumu.

Alisema Tanzania kama zilivyo jamii zingine duniani inakabiliwa na tatizo la ukatili wa kijinsia na kuwa ukatili huo hauchagui kabila, dini, nafasi ya mtu wala rangi yake bali ni hulka ya mtu jambo ambalo limekuwa gumu kulitokomeza.

Alisema takwimu zinazotokana na utafiti wa Afya hapa nchini za mwaka 2010 zinaonesha asilimia 39 ya wanawake wote Tanzania wameathirika kwa namna moja au nyingine na ukatili wa kimwili tokea wakiwa na umri wa miaka 15.

Alisema pia asilimia 33 ya wanawake hao wameathirika na vitendo vya ukatili kati ya mwaka 2009 na 2010.

Alisema serikali inatambua kuhusu jambo hilo na kuwa ili ifanye kazi yake vizuri ni muhimu kwa kila mmoja kutambua matokeo hasi ya ukatili wa kijinsia na kuchukua hatua za kusema 'UKATILI WA KIJINSIA SASA BASI' na kuthubutu kukemea na kukataa aina yoyote ya ukatili wa kijinsia.

No comments:

Post a Comment