TANGAZO


Saturday, December 21, 2013

Mtanange wa Kombe la Nani Mtani Jembe katika picha Uwanja wa Taifa

*Simba yaifunza Yanga Soka
*Yaipiga 3-1, mchana kweupe
 
Kikosi cha Simba kilichojitupa Uwanja wa Taifa dhidi ya Yanga katika mchezo wa Nani Mtani Jembe leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
 Kikosi cha Yanga kilichojitupa Uwanja wa Taifa dhidi ya Simba katika mchezo wa Nani Mtani Jembe leo.
Mashabiki wa Yanga wakiwa tayari kufuatilia mchezo kati ya timu yao hiyo, dhidi ya Simba wakati wa mchezo huo wa watani wa jadi.
Mashabiki wa Simba wakifuatilia mchezo kati ya timu yao hiyo, dhidi ya Yanga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.




Mashabiki wa Simba wakionesha mabango yenye ujumbe mbalimbali kwa watani wao, Yanga wakati wa mchezo huo.
Amisi Tambwe akishangilia bao la kwanza aliloifungia timu yake ya Simba dhidi ya Yanga katika mchezo wa kombe la Nani Mtani Jembe, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Wachezaji wa Simba wakishangilia bao la kwanza la timu hiyo lililofungwa na Amis Tamwe dhidi ya Yanga wakati wa mchezo wa Nani Mtani Jembe, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Simba ilishinda mabao 3-1.
Wachezaji wa Simba wakishangilia bao la kwanza la timu hiyo lililofungwa na Amis Tamwe dhidi ya Yanga wakati wa mchezo wa Nani Mtani Jembe, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Simba ilishinda mabao 3-1.
 Uhuru Selemani akimtoka Mbuyu Twite wa Yanga wakati wa mchezo huo.
  Uhuru Selemani akijaribu kumtoka Mbuyu Twite wa Yanga wakati wa mchezo huo.
 Ramadhani Singano 'Messi wa Simba', akijaribu kumpiga chenga David Luhende wa Yanga.
  Ramadhani Singano 'Messi wa Simba', akimtoka David Luhende wa Yanga.
Golikipa wa Yanga, Juma Kaseja akiwa amekaa chini baada ya kufungwa bao la pili na Amisi Tembwe wa Simba, wakati wa mchezo huo.
Amisi Tambwe, akishangilia bao lake la pili kwa timu yake ya Simba dhidi ya Yanga, wakati wa mchezo huo.
Amisi Tambwe, akiwakebehi mashabiki wa Yanga, wakati akishangilia bao lake la pili kwa timu yake ya Simba dhidi ya timu hiyo.




Ubao wa matangazo ukionesha Simba mabao 2 na Yanga 0 hadi mapumziko.
Mashabiki wa Simba wakipuliza filimbi na vuvuzela zao baada ya timu yao hiyo, kuachia kipigo Yanga mabao 2 kwa 0 hadi mapumziko.
Uhuru Selemani wa Simba akiutuliza mpira kifuani huku akiangaliwa na Didier Kavumbagu wa Yanga.
David Luhende wa Yanga akiudhibiti mpira uliokuwa ukiwaniwa pia na Awadh Juma (kulia) wa Simba.
David Luhende wa Yanga (kushoto), akiwania mpira na Awadh Juma wa Simba.
Awadh Juma wa Simba (kulia), akijaribu kuwatoka Kelvin Yondani (katikati) na Didier Kavumbagu wote wa Yanga, wakati wa mchezo wa Nani Mtani Jembe uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Awadh Juma (kulia) wa Simba akipiga mpira na kuwapita wachezaji Kelvin Yondani (kushoto) na Didier Kavumbagu (18), wote wa Yanga.

Mashabiki wa Yanga wakiwa hawaamini macho yao kwa kilichotoke baada ya timu yao ya Yanga kupata kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa mtani wake wa jadi, Simba, wakati wa mchezo wa Nani Mtani Jembo, uliotayarishwa na TBL, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Makocha wa Yanga Brandts (kulia) na Fred Minziro, wakijadili jambo wakati wa filimbi ya mapumziko baada ya kufungwa mabao 2-0 mpaka wakati huo.
Kocha wa Simba akiwa na wachezaji wake wakitola uwanjani wakati wa mapumziko, wakati mchezo huo.


Awadhi Juma wa Simba akishangilia bao leke aliloifungia timu yake ya Simba, likiwa ni bao la 3 dhi ya Yanga.


 
 




Wachezaji wa Simba wakivalishwa medali na Rais wa TFF, Jamali Malinzi.



Jerryson Tegete wa Yanga, akipokea kikombe cha ushindi wa pili kwa timu yake hiyo.
Nahodha wa Simba, Haruna Shamte akikabidhiwa Kombe la Ubingwa wa Nani Mtani Jembe na Waziri wa Katiba na Sheria, M. Chikawe.
Haruna Shamte, akilinyanyua juu Kombe hilo.
Wachezaji na viongozi wa timu ya Simba, wakipiga picha ya pamoja na kombe lao hilo.
 Wachezaji wa Simba wakishangilia kombe la ubingwa katika mchezo wa Nani Mtani Jembe, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Simba ilishinda mabao 3-1.
Wachezaji wa Simba wakishangilia kombe la ubingwa katika mchezo wa Nani Mtani Jembe, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Simba ilishinda mabao 3-1.
Kocha wa Simba, Lugarusic, akifurahi na wachezaji wake mara baada ya kukabidhiwa Kombe la Nani Mtani Jembe, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Golikipa wa Simba Yaw Barko, akiwa amelishikilia kombe la Nani Mtani Jembe baada ya timu yake hiyo kuifunga Yanga mabao 3-1 katika mchezo huo.

No comments:

Post a Comment