TANGAZO


Wednesday, December 18, 2013

Msanii wa muziki wa bongo fleva, Remmy Williams atua nchini


Msanii wa muziki wa bongo fleva Remmy Williams, akiwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, mara baada ya kuwasili nchini leo, akitokea nchini Italy. (Picha zote na Super D, Mnyamwezi)

MSANII wa mziki wa bongo fleva Remmy William (kushoto) akiwasili nchini akitokea Italy kulia ni meneja wake nchini Italy Wactor Fizio walipowasili nchini Tanzania.

MSANII wa mziki wa bongo fleva Remmy Williams.
MSANII wa mziki wa bongo fleva Remmy Williams katikati akilakiwa na baadhi ya warembo waliojitokeza kumpokea msanii huyo.

Msanii wa muziki wa bongo fleva, Remy Williams akiwa ameshikwa mkono na Meneja  wake wa Tanzania Mcdennis Mgatha, mara baada ya kuwasili nchini akitokea nchini Italy leo.
Msanii William anayefanyashughuli zake za muziki nchini Italy ameingia nchini leo na kutua jijni Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya kazi na wasanii wenzake nchini.

Akizungumzia ujio wake mara baada ya kutua uwanja wa ndege wa  Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es salaam amesema kuwa nawapenda wasanii wote wa Tanzania wanavyofanya vema nchini na kazi zao nyingi zinavuka mipaka kwa ajili ya kujitangaza kimataifa,  hata  hivyo yeye amejitokeza kuupaisha mziki huo kwa kushirikiana na wasanii atakaochaguliwa kushirikiana naye.

Akizungumzia ujio wa msanii huyo meneja wake nchini Mcdennis Mgatha amesema msanii huyo kaja nchini kwa ajili ya kufanya colab na wasanii hapa nchini hivyo wapenzi wa muziki wakae mkao wa kula kwani ana vitu vingi sana alivyo waandalia ikiwemo nyimbo mpya pamoja na kufanya shoo kwa ajili ya kutambulisha nyimbo hizo

No comments:

Post a Comment