Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi (Kati kati) akiongoza Mkutano Maalum wa Baraza Kuu la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma
Katibu wa Chama cha Walimu Bw.Ezekiel Oluoch akitoa mchango wake mkutano huo
Katibu wa Bodi ya Mishahara Bi. Tamika Mwakahesya akitoa mchango wake katika mkutano.
Katibu wa Sekretariati ya Ajira bw. Xavier Daudi akitoa mchango wake katika mkutano.
Katibu wa TUGHE Bw. Ally Kiwenge akitoa maoni yake katika mkutano.
Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu Prof. Sifuni Mchome akijitambulisha kwa wajumbe wa mkutano ika mkutano
Moja kati ya mada zilizowasilishwa katika mkutano kuhusu muundo wa utumishi wa walimu unaotumika hivi sasa
Na Mwandishi wetu
OFISI ya Rais Menejementi ya Utumishi wa Umma, imeitisha
Mkutano maalum wa Baraza Kuu la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma ili kupata
mrejesho kuhusu masuala yanayowagusa watumishi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma Bw. George D. Yambesi akifungua mkutano huo, mjini Dodoma leo, amesema mkutano
huo, maalum unafuatia maagizo yaliyotolewa katika mkutano uliopita.
“Kati ya yale yaliyosisitizwa na kukubalika ni kuitisha
Mkutano Maalum wa Baraza kwa ajili ya kujadili Muundo wa Maendeleo ya Utumishi
wa Walimu na masuala mengine muhimu yanayohitaji ushauri wa Baraza”, Bw. Yambesi
alisema.
Bw. Yambesi, ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza hilo
alisema baraza limeundwa kisheria kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha sheria ya
Majadiliano ya Pamoja katika Utumishi wa Umma, Na. 19 ya mwaka 2003, ambapo
jukumu lake kubwa ni kuishauri Serikali kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu
ustawi wa watumishi wa umma ikiwa ni pamoja na utumishi wao. Utumishi wa Umma
unasimamiwa na sheria, Kanuni na Taratibu mbalimbali. Hivyo, Baraza linao
wajibu wa kushauri kuhusu miongozo mbalimbali inayosimamia Utumishi wa Umma.
Katibu Mkuu Bw. Yambesi alisema serikali inapenda kupata
maoni ya wajumbe wa baraza kuhusu Tathmini ya utekelezaji wa Waraka wa Mkuu wa
Utumishi wa Umma Na. 1 wa mwaka 2000 unaohusu watumishi wa umma kujiunga na
Siasa.
Alifafanua kuwa kwa sababu tunatarajia kuwa na uchaguzi
wa Serikali za Mitaa mwakani na huenda baadhi ya watumishi wa Umma wakapenda
kugombea nafasi za uongozi wa kisiasa ambapo utaratibu uliopo sasa uliandaliwa
miaka kumi na tatu (13) iliyopita, hivyo kuwepo umuhimu wa kupima kama bado
unakidhi matarajio.
Pamoja na wajumbe wa baraza, katika mkutano huo maalum ulihudhuriwa
na wawakilishi kutoka mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Taasisi mbalimbali ndani ya
Utumishi wa Umma.
No comments:
Post a Comment