TANGAZO


Tuesday, December 10, 2013

Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal aongoza Dhifa ya Kitaifa, Ikulu jijini Dar es Salaam



Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, wakati wa dhifa ya kitaifa iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimia na mmoja wa Mabalozi waliofika kwenye dhifa hiyo.

Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Zambia, mama Judith Kangoma.

Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na Mbunge wa Busega, Dk. Titus Kamani.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel. Kulia ni  Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Maelezo, Assah Mwambene. 

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na Balozi wa Canada nchini, Alexandre Leveque.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa, Elisante Ole Gabriel, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick.

Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka.Kushoto aliyekaa ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein.

Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salim akibadilishana mawazo na  Mbunge wa Busega, Dk. Titus Kamani.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na mmoja wa wageni waalikwa kwenye dhifa iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akimuelekeza jambo Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, wakati wakiangalia kikundi cha ngoma kilichokuwa kikitumbuiza wageni.
Kikundi cha ngoma ya Amayaga kutoka Kagera 
kikitumbuiza.

Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal (wa pili kulia), akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, wakiangalia ngoma za jadi. Kushoto  ni mke wa Dk. Bila, mama Asha Bilal na kushoto mwisho ni mke wa Dk. Shein, mama Mwema Shein.

Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Uratibu wa Vyombo vya Habari cha Idara ya Habari (MAELEZO), Jamali  Zuber akiwa na wenzake wakiangalia ngoma za asili.

Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal (kulia) akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein wakiwa wamepumzika kwenye dhifa hiyo. (Picha zote na Hussein Makame)

No comments:

Post a Comment