Majeshi ya Sudan Kusini yanajiandaa kupambana na waasi katika
mji wa Bor, Rais Salva Kiir amesema.
Rais Kiir ameliambia bunge la nchi hiyo kwamba majeshi yapo tayari na
kuongeza kuwa mashambulizi yalichaleweshwa ili kuruhusu raia wa Marekani
kuondolewa katika eneo hilo.Takribani wiki imepita tangu mapigano ya kikabila yaanze na kusababisha hofu kwa raia. Maafisa ya shirika la misaada wamelielezea eneo hilo kuwa na matukio ya umwakigaji damu pamoja na mauaji.
Mapema Majeshi ya Sudan Kusini yamethibitisha kuwa Bentiu, mji wenye utajiri wa mafuta katika jimbo la Unity limeangukia mikononi mwa wapiganaji wanaoungwa mkono na Makamu wa Rais aliyestaafu Riek Machar.
Rais Kiir, kutoka kabila kubwa nchini humo la Dinka, mwezi julai alimfuta kazi Bwana Machar anatokea jamii ya Nuer.
Rais Kiir anamtuhumu Bwana Machar kwa kufanya jaribio la kumpindua, jambo linalopingwa vikali na Machar.
No comments:
Post a Comment