TANGAZO


Wednesday, December 4, 2013

Kinana kusaidiana na Dk. Mwakyembe kusuluhisha mgogoro wa TAZARA

 

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia), akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara), Stesheni ya Mbeya, akiwa katika ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM jijini Mbeya. Kinana alisikiliza kero mbalimbali kutoka kwa uongozi pamoja na wafanyakazi ambapo aliahidi kusaidiana na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe kuzitafutia ufumbuzi kwa kuzipeleka ngazi za juu kuzijadili.

Mfanyakazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara), Stesheni ya Mbeya, Herry Mutashobya akizungumza mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (hayupo pichani), kuhusu hujuma mbalimbali zinazofanyiwa Tazara. Jumla ya kero 35 aliambiwa Kinna na wafanyakazi hao.

Mfanyakazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara), Stesheni ya Mbeya, Gerald Simiko akizungumza mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (hayupo pichani), ambapo alilalamikia kitendo cha uongozi wa mamlaka hiyo, kuwatesa wanaostaafu kwa kutowapatia stahili ya mafao yao wanapostaafu kazi. Kinana alifanya mkutano huo wa kusikiliza kero za wafanyakazi hao katika Stesheni ya Mbeya leo.
Kinana akihutubia katika mkutano huo na wafanyakazi
Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, ambaye pia ameteuliwa na Rais kuwa Mbunge, Asha Rose Migiro (kushoto) akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya D, Mary Mwanjelwa wakati wa mapokezi ya msafara wa Kinana, katika Kijiji cha Iwambi, Kata ya Iwambi, Mbeya Mjini leo.

Kinana akisalimiana na wanachama wa CCM wakati wa mapokezi katika Kata ya Iwambi, Mbeya Mjini leo.

Kinana akitoka baada ya kuzungumza na wafanyakazi wa Tazara, Mbeya leo.
Kinana akizungumza na wanachama wa CCM waliofika kumlaki katika Kata ya Iwambi Mbeya Mjini.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akiwa na Kada wa CCM, Charles Mwakipesile wakati wa mapokezi ya msafara wa Kinana katika Kata ya Iwambi, Mbeya Mjini leo.
NAPE akiwa amekaa na baadhi ya wananchama wa Shina namba 7 la CCM Iyunga, Mbeya Mjini. (Picha zote na Kamanda Richard Mwaikenda)

No comments:

Post a Comment