TANGAZO


Wednesday, December 11, 2013

India yapinga wapenzi wa jinsia moja

 


Maandamano ya wapenzi wa jinsia moja India
Mahakama ya juu kabisa nchini India, imetaka kuendelea kwa sheria inayowatia hatiani wapenzi wa jinsia moja, uamuzi ambao unaonekana kuwa pigo kwa haki za watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.
Uamuzi wa mahakama hiyo unabadilisha uamuzi wa Mahakama Kuu ya Delhi uliofanyika mwaka 2009, ambapo mahakama hiyo iliona si uvunjaji sheria kwa watu wanaoshiriki vitendo vya wapenzi wa jinsia moja.

 
Mahakama hiyo ya juu imesema ni jukumu la bunge kutunga sheria kuhusu suala hilo.
Kwa mujibu wa kifungu cha 377, sheria ya kikoloni iliyodumu nchini India kwa miaka 153, uhusiano wa kimapenzi kwa wattu wa jinsia moja ni kosa lisilo la kawaida na adhabu yake ni kifungo cha miaka kumi jela.
Vyama kadha vya kisiasa, makundi ya kijamii na kidini nchini India, katika mkesha wa kutolewa hukumu juu ya suala la wapenzi wa jinsia moja, mwaka 2009, waliitaka mahakama hiyo kuendelea na sheria inayopiga marufuku vitendo vinavyowashirikisha wapenzi wa jinsia moja.
Vyombo vya habari vinasema japokuwa sheria hiyo ndra ilitumika, kama iliweza kutumika kuwashitaki watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia, mara kwa mara sheria hiyo ilitumiwa na polisi kuwanyanyasa wapenzi wa jinsia moja. Pia kwa India iliyojikita katika utamaduni na mila, uhusiano wa jinsia moja ni mwiko na watu wengi wanaona uhusiano wa jinsia moja si halali.
'Ni siku ya giza'"Ni juu ya bunge kutunga sheria kuhusu suala hili," Jaji GS Singhvi, mkuu wa jopo la majaji wawili wa Mahakama ya juu kabisa nchini India, amesema katika kutoa hukumu ya Jumatano, ambayo imetolewa katika siku yake ya mwisho kabla ya kustaafu.

No comments:

Post a Comment