akimkaribisha mgeni rasmi katika hafla ya kufunga mafunzo ya
watoa huduma za Afya ya uzazi wa mpango yaliyokuwa
yakifanyika katika kijiji cha Ikwiriri wilayani Rufiji mapema
hivi karibuni. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya UMATI Taifa na
Mratibu wa huduma za afya ya uzazi Taifa katika ngazi ya jamii
Bi Rose Wasira. (Picha zote na Frank Shija - Maelezo)
Mwenyekiti wa Bodi ya UMATI Taifa na Mratibu wa huduma za afya ya uzazi Taifa katika ngazi ya jamii Bi Rose Wasira akisisitiza jambo kwa wahitimu wa mafunzo ya utoaji huduma za uzazi wa mpango hawapo pichani alipokuwa mgen rasmi wakati wa hafla ya kufunga mafunzo hayo hivi karibuni katika kijiji cha Ikwiriri wilayani Rufiji.Kushoto ni Meneja wa UMAI Kanda ya Mashariki Dk. Martin Sinje na kulia ni Mratibu wa afya ya uzazi wa mpango(w) Rufiji Bi Gloria Mshana.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya utoaji wa huduma za
afya ya uzazi wa mpango wakifuatilia kwa makini hotuba ya
mgeni rasmi(hayupo pichani)wakati wa hafla ya kufunga
mafunzo hayo iliofanyika kijijini Ikwiriri wilayani Rufiji
mapema hivi karibuni.
Mratibu wa afya ya uzazi wa mpango (W), Rufiji Bi Gloria
Mshana akifafanua jambo kwa wahitimu wa mafunzo ya utoaji
huduma za uzazi wa mpango(hawapo pichani) kushoto ni
Mwenyekiti wa Bodi ya UMATI Taifa ambaye pia Mratibu wa
huduma za afya ya uzazi Taifa katika ngazi ya jamii Bi. Rose
Wasira.
Mwenyekiti wa Bodi ya UMATI Taifa na Mratibu wa huduma za afya ya uzazi Taifa katika ngazi ya jamii Bi Rose Wasira akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya utoaji wa huduma za afya ya uzazi wa mpango yaliyofanyika katika kijiji cha Ikwiriri wilayani Rufiji mapema hivi karibuni.
Mratibu wa Mradi wa uwiano katika ubunifu wa kuboresha afya ya mama na mtoto kanda ya Mashariki Anthony Mkinga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya utoaji wa huduma ya afya ya uzazi wa mpango mara baada ya kukabidhiwa vitendea kazi katika hafla iliyofanyika kijijini Ikwiriri wilayani Rufiji mapema hivi karibuni.
Na Frank Shija-Maelezo
UMATI imepongezwa kwa kuendelea kuwa asasi bora
katika kutoa huduma ya Afya ya uzazi wa mpango hapa nchini.
Pongezi hizo, zimetolewa na Mratibu wa Huduma za Uzazi
wa Mpango Kitaifa katika ngazi ya Jamii, Bi. Rose Wasira, lipokuwa akifunga mafunzo
ya watoa huduma na usambazaji wa dawa za afya ya uzazi wa mpango
kutoka Kata za Bungu na Chumbi wilayani Rufiji mapema hivi karibuni.Katika hotuba yake Wasira alisema kuwa UMATI nimiongoni mwa asasi chache zinazosaidia jamii hususan katika suala zima la afya ya uzazi wa mpango .na kuelezea kufurahishwa kwake na mradi huu mpya ambao utaongeza upatikanaji wahuduma bora za afya ya uzazi wa mpango miongoni mwa jamii.
“Niseme wazi UMATI mnafanyakazi nzuri hongereni sana
ata Serikali inatambua mchango wenu kwa jamii endeleeni na moyo huu nasi tutaendelea
kushirikiana nanyi katika kuhakikisha mnatekeleza majukumu yenu katika mazingira
mazuri.”Alisema Bi.Wasira
Mafunzo hayo yamefanyika ikiwa nimaandalizi ya utekelezaji
wa mradi
Kwa upande wake Meneja wa UMATI Kanda ya Mashariki Dk.Martin
Sinje amesema kuwa baada ya kubaini kuwa wanaume awashiriki kikamilifu katika afya
ya uzazi wa mpango wamebuni mradi ambao utaboresha huduma ya afya ya uzazi wa mpango
kwa jamii.
Dkt. Martin aliongeza kuwa kufuatia kuanza kutekelezwa
kwa mradi huo ushiriki wa wanaume katika suala zima la afya ya uzazi utaongezeka.Wakati huo huo mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo ameishukuru UMATI kwa kuwapa mafunzo hayo na kusisitiza kuwa watakuwa chachu ya mabadiliko miongoni mwa jamii wanazotoka.
Mradi wa uwiano katika ubunifu wa kuboresha afya ya mama na mtoto umelenga kuleta uwiano sawa katika ushiriki na utumiaji wa huduma za afya ya uzazi kwa jamii,ambapo mradi huu utatekelezwa katika ya wilaya za Mlele na Mpanda mkoani Katavi na Rufiji Mkoani Pwani unafadhiliwa na Kampuni ya kusamba za dawa za uzazi wa mpango inayoitwa Merck Sharp and Dome (MSD).
No comments:
Post a Comment