TANGAZO

Thursday, November 21, 2013

Picha mbalimbali za Babu Seya na mwanawe, Papii Kocha, walipokuwa Mahakama ya Rufaani jijini Dar es Salaam leo

Baadhi ya waandishi wa habari pamoja na wananchi wakiwa Mahakama ya Rufaa Tanzania kufuatilia kesi Mwanamuziki Nguza Viking 'Babu Seya' na mtoto wake, Papii Nguza 'Papii Kocha', wakati wa kutolewa uamuzi wa rufani yao, waliyokata kupinga adhabu ya kifungo cha maisha wanayoitumikia. Hata hivyo, uamuzi uliotolewa ni kutupwa kwa rufaani hiyo na hivyo kurejeshwa Gerezani kuendelea na adhabu hiyo.

 Babu Seya na mwanawe, Papii Kocha wamemuomba Rais Jakaya Kikwete kuwapa msamaha na hatimaye waweze kuwa tena huru. 

Aidha, wamesema kuwa wao, hawakutenda kosa hilo, walililohukumiwa nalo na kama wamefanya basi Mwenyezi Mungu atawahukumu. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)

Papii Nguza, akiwapungia wananchi pamoja na ndugu wa familia yao, waliofika Mahakama ya Rufaa kufuatilia hukumu ya rufani yao, huku baba yake, Nguza Vicking 'Babu Seya akiongozwa na askari Magereza kutoka katika chumba cha Mahakama hiyo baada ya kutolewa uamuzi wa kutupwa kwa rufani yao na kisha kurejeshwa Gerezani kuendelea na kifungo chao cha maisha. 
Mwanamuziki Nguza Viking 'Babu Seya' na mtoto wake, Papii Nguza 'Papii Kocha', wakiwapungia, ndugu, marafiki pamoja na wananchi waliofika Mahakama ya Rufaa Tanzania, kufuatilia uamuzi wa rufaani yao, uliokuwa uliotolewa leo, mahakamani hapo. Babu Seya na mwanawe, Papii Kocha walirejeshwa Gerezani kuendelea na adhabu yao baada ya kutupiliwa mbali rufani yao ya kupinga adhabu ya kifungo cha maisha.
 Picha mbalimbali juu na chini ya Mwanamuziki Nguza 'Babu Seya na mwanawe, Papii Kocha wakiwa pungia na kuwaaga ndugu, jamaa, marafiki na wananchi mbalimbali waliofika mahakamani hapo leo, kufuatilia uamuzi wa rufaani yao hiyo.
 
Mwanamuziki Nguza Viking na mtoto wake, Papii Nguza wakiwa kwenye gari la Magereza baada ya rufani yao waliyokata kupinga adhabu ya kifungo cha maisha wanayoitumikia kutupwa katika Mahakama ya Rufaani ya Tanzania, Dar es Salaam leo.

 Wananchi wakifuatilia tukio la kuondoka mahakamani hapo, wanamuziki hao.
 Waendesha bodaboda wakishangaa tukio hilo.
Hapa wananchi pamoja na waendesha bodaboda wakiulizana kulikoni katika uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Rufaani Tanzania kwa wanamuziki hao.
Wananchi wakishangaa kuwaangalia wanamuziki hao wakiwa kwenye karandinga la Magereza wakirejeshwa Gerezani leo.

No comments:

Post a Comment