Na Hassan Silayo
Kampuni ya Pan African Energy
inayoendelea na Ukarabati wa visima vya gesi imefanikiwa kukamilisha takriban
asilimia 85 ya matengenezo katika visima vya gesi vya songosongo.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba
wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam.
Mhandisi Mramba alisema kuwa
matengenezo hayo ambayo yanategemewa kukamilika November 26 mwaka huu yameonesha
mafanikio ikiwa ni pamoja na kuwa na kasi ya kuridhisha kuliko ilivyotegemewa
kwa kipindi cha mda mfupi tangu matengenezo hayo yaanze.
“kwa kweli napenda kuwaambia
watanzania kuwa wenzetu wa Pan African wanaoendelea na ukarabati katika visima
vya songosongo wamekuwa na kasi ya kuridhisha ambapo mpaka sasa wamekamilisha
kiasi asilimia 85 ya matengenezo na tunatarajia mapaka kufikia leo jioni
tutaweza kuleta asilimia 80 ya gesi na kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la
umeme hasa katika kipindi hiki cha ukarabati wa visima hivyo.
Aidha Mhandisi Mramba alifafanua kuwa
matengenezo hayo ambayo yalienda sambamba na kuzima mitambo kwenye visima hivyo
yanafanyika kila mwaka ili kuboresha uzalishaji wa umeme kwa kutumia
gesi.
Akijibu swali la waandishi wa habari
waliotaka kujua kuhusu vigezo va ugawaji wa umeme hasa katika kipindi hiki cha
matengenezo Mhandisi alisema kuwa maeneo muhimu kama kwenye mahospitali na
sehemu za usalama yanapewa kipaumbele kutokana na umuhimu wake katika
jamii. (Habai, Picha zote na
No comments:
Post a Comment