Jeneza lenye mwili wa marehemu Dk. Sengondo Mvungi, likiwasili kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo, kwa ajili ya kuagwa.
Jeneza likipelekwa sehemu iliyoandaliwa kwa ajili ya kuagia.
Ndugu na jamaa, wakipeleka mashada ya maua na picha ya marehemu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati alipokuwa akitoa salamu za rambi rambi za Serikali wakati wa shughuli za kuuaga mwili wa marehemu Dk. Sengondo Mvungi, kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais, Dk. Gahlib Bilali, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Rais mstaafu Benjamin Mkapa, Waziri Mkuu mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Katiba Jaji Joseph Warioba, Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Anjela Kairuki na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, wakiwa katika shughuli za kuuaga mwili wa marehemu, Dk. Sengondo Mvungi, kwenye Viwanja vya Karimjee jijini, Dar es Salaam leo.
Viongozi wa dini ya Kikristo, wakiongoza misa, wakati wa shughuli hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Dk. Sengondo Mvungi, wakati wa shughuli ya kuuagwa mwili huo, iliyofanyika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Dk. Sengondo Mvungi, wakati wa shughuli ya kuuagwa mwili huo, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na OMR)
No comments:
Post a Comment